Desemba
29, 2021.
------------------------------------------------
JUMATANO,
OKTAVA YA NOELI
Somo
la 1: 1Yn 2: 3-11 Yohane anatuambia kwamba hatuwezi kumfahamu Yesu hadi
tumeshika amri zake: kumpenda Mungu na jirani.
Wimbo
wa katikati: Zab 95: 1-3,5-6 Mwimbieni Bwana wimbo mpya, tangazeni wokovu wake
siku kwa siku na maajabu yake kati ya watu.
Injili:
Lk 2: 22-35 Luka anatuambia kuhusu kutolewa kwa mtoto Yesu hekaluni, na Simeon
anatabiri kwamba upanga utapenya katika moyo wa Maria Mama yake Yesu.
------------------------------------------------
UWEPO
WA MUNGU KATI YETU!
Liturjia
ya leo inatabiri kuhusu wakati uliopita lakini pia inatabiri muda mfupi ujao.
Ni siku chache tu zilizopita tumesheherekea kuzaliwa kwa Yesu, na furaha ya
sikukuu hii haiwezi kuisha. Katika somo la Injili tunamuona Simeoni nabii. Mtu
huyu Mtakatifu alikuwa ameandaliwa na Mungu kwa ufunuo wake mwenyewe kwamba
angemuona Masiha kwa macho yake, mkombozi wa ulimwengu. Siku zote za maisha
yake amekuwa akitarajia hili. Alitamani na kusubiri kwa siku hii. Pale tu Maria
na Yosefu walipo mpeleka mtoto Yesu hekaluni Simeoni alitambua ndani ya moyo
wake kwamba mtoto huyu ndiye Mkombozi tuliye ahaidiwa. Maneno yake yana nguvu.
Anasema “Bwana waweza kumruhusu mtumishi wako aende kwa Amani..kwa macho yangu
nimeuona wokovu utokao kwako..” Simeoni alitambua kwamba maisha yake sasa
yalikamilika. Alikuwa tayari sasa kufa kwani alipewa upendeleo wa kumuona
Kristo. Alimshika mikononi mwake akampa Mungu utukufu kwa wakati ule.
Mtoto
aliyeshikwa na Simeoni ni Mungu kweli kweli. Lakini alikuwa Mungu katika mwili
wa mtoto mdogo. Simoni hakika alimuona kwa jinsi alivyokuwa na kufurahi.
Tunapaswa kutambua uwepo wa Masiha na kuufurahia kama Simeoni. Yesu yupo hai
kwa kila moyo tunaopewa na Mungu, katika kila sakramenti ya kanisa, kwa kila
somo la Maandiko matakatifu, na yupo ndani ya mioyo yetu. Mioyo yetu inapaswa
kuwa hilo hekalu ambalo tunatambua uwepo wa Kristo ndani yake na tunapaswa kufurahi
kwa kuwa karibu nasi namna hii.
Leo
antifona ya wimbo wa kwanza inatupa sababu yote-Mungu mwana asingefanyika mwili
hata kidogo kama isingekuwa ni upendo wa Mungu Baba kwetu sisi. “Mungu
aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwanae ili wote wanao mwamini wasipotee
bali wawe na uzima wa milele”. Jukumu letu ni kukubali ujumbe huu na upendo
unaojengeka ndani yake. Kama kuna mtu ambaye alitambua jinsi ya kupokea zawadi
hii ni Maria, na Simeoni pia. Maria alikuwa ni wa kwanza wa kupokea zawadi ya
Mungu, na akajibu kwa upendo na kujiamini na kujikabidhi kwake. Simoni
alimpokea mtoto mikonini mwake akamshukuru Mungu…Macho yangu yameuona wokovu
ulioandaa kwa watu wote waweze kuuona.
Sala:
Bwana, ninakushukuru kwa zawadi ya Mwanao ulimwenguni. Tunaomba tupokee zawadi
hii kwa mioyo yetu yote. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment