MASOMO
YA MISA DESEMBA 29, 2021
SIKU
YA TANO YA OCTAVA YA KUZALIWA BWANA
SOMO
1
1Yoh.
2:3-11
Wapenzi,
Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua Yesu, ikiwa tunashika amri zake, Yeye
asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani
yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika
kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa
anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
Wapenzi,
siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo
amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia.
Tena
nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na yenu; kwa kuwa giza
linapita na vile nuru ya kweli imekwisha kung’aa. Yeye asemaye kwamba yumo
nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. Yeye ampendaye ndugu
yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. Bali yeye amchukiaye
ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa
sababu giza imempofusha macho.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
96:1-3,5-6 (K) 11a
(K)
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni
Bwana, nchi yote,
Mwimbieni
Bwana, libarikini jina lake. (K)
Tangazeni
wokovu wake siku kwa siku,
Wahubirini
mataifa habari za utukufu wake,
Na
watu wote habari za maajabu yake. (K)
Lakini
Bwana ndiye aliyezifanya mbingu,
Heshima
na adhama ziko mbele yake,
Nguvu
na uzuri zimo katika patakatifu pake. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Siku
takatifu imetung’aria: Enyi mataifa, njoni mkamwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga
mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.
INJILI
Lk.
2:22-35
Kisha,
zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa, walikwenda na
Yesu hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua
mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana, wakatoe na sadaka, kama
ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili.
Na
tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Yerusalemu palikuwa na mtu,
jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya
Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Naye alikuwa ameonywa na Roho
Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Basi akaja
hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili
wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, yeye mwenyewe alimpokea mkononi
mwake, akamshukuru Mungu, akisema, Sasa Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa
Amani kama ulivyosema kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, uliouweka
tayari machoni pa watu wote; nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, na kuwa utukufu
wa watu wako Israeli.
Nababye
na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Simeoni
akawabariki akawaambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na
kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Naye
mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment