“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Desemba 16, 2021
Juma
la 3 la Majilio
Isa
54: 1-10;
Zab
30: 2-13;
Lk
7: 24-30
UNA
MWALIKO WA UFALME WA MUNGU!
Ni
nani aliye mkuu katika Ufalme wa Mbinguni? Yesu anamsifia Yohane kuwa mkuu kati
ya uzawa wa wanawake! Lakini katika hali hiyo hiyo Yesu anasema aliye mdogo
katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohane! Hii inaonekana kama vile
inachanganya kama tusipo elewa Yesu alitaka kukamilisha nini kwa ajili yetu!
Yohane ni wa mwisho na mkuu kati ya manabii wa Agano la kale. Alikamilisha kazi
zote muhimu za manabii-kumuonesha Yesu, Mwana-kondoo wa Mungu na Masiha. Yohane
alimuonesha Yesu katika mto Yordani “tazama Mwana-kondoo wa Mungu aondoaye dhambi
za dunia” (Yn 1:29). Yohane aliona kwa mbali kile Yesu ambacho atakikamilisha
kwa kifo chake pale Msalabani-ukombozi wetu kutoka katika bonde la dhambi na
mauti na kutufanya wana wa Mungu na raia wa Mbinguni.
Kama
Yohane, sisi pia tunaitwa tutoe ushahidi wa maisha ya mwanga na ukweli kama
Yesu Kristo. Sisi tunaitwa kuwa wafuasi wa Yesu. Tunaitwa kuitikia wito kwa
kukubali mafundisho na ukombozi uliotolewa na Yesu ili tupokee mwaliko wa
ufalme wa Mbinguni. Tunaweza kupatwa na kishawishi cha kujiona wema kama wale
viongozi wa dini kipindi cha Yesu na kukosa mwaliko wa Yesu. Usikatae mwaliko
wake, bali upokee kwa moyo wote. Katika kuupokea kwa moyo wote, utashangaa
Mungu atakubariki hata katika hali ambayo huwezi kuelezea.
Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuingia katika mwaliko wako kila siku katika maisha
yangu. Ninaomba kila wakati nichague mapenzi yako matakatifu na niyaishi bila
kujibakiza. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment