MASOMO
YA MISA, DISEMBA 16, 2021
ALHAMISI
, JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
54:1 – 10
Imba,
wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe
usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake
yeye aliyeolewa, asema Bwana. Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia
ya maskani yako; usiwakataze; ongoeza urefu wa Kamba zako; vikaze vigingi vya
hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao
wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
Usiogope;
maana hutatahayarika; wala usifadhaike; maan ahutaaibishwa; kwa kuwa utaisahau
aibu ya ujana wako, pia mashutumu ya ujana wako hutayakumbuka tena. Kwa sababu
Muumba wako ni mume wako; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa
Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Maana
Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa
ujana, atupwapo, asema Mungu wako. Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa
rehema nyingi nitakukusanya. Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu
dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi
wako.
Kwa
maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuru kwangu; maana kama nilivyoapa ya
kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba
sitakuonea hasira, wala kukukemea. Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa;
bali wema wangu hautaondoka kwake, wala agano langu la Amani halitaondolewa;
asema Bwana akurehemuye.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
30:1, 3 – 5, 10 – 12 (K) 1
(K)
Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua.
Ee
Bwana, nitakutukuza, kwa maana umeniinua,
Wala
hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
Umeniinua
nafsi yangu,
Ee
Bwana, kutoka kuzimu.
Umenihuisha
na kunitoa
Miongoni
mwao washukao shimoni. (K)
Mwimbieni
Bwana zaburi,
Enyi
watauwa wake.
Na
kufanya shukrani.
Kwa
kumbukumbu la utakatifu wake.
Maana
ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,
Aktika
radhi yake mna uhai.
Huenda
kilio huja kukaa usiku,
Lakini
asubuhi huwa furaha. (K)
Ee
Bwana, usikie, unirehemu,
Bwana,
uwe msaidizi wangu.
Uligeuza
matanga yangu kuwa machezo;
Ee
Bwana, Mungu wangu,
Nitakushukuru
milele. (K)
SHANGILIO
Lk.
3:4, 6
Aleluya,
aleluya,
Itengenezeni
njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake, na wote wenye mwili watauona wokovu wa
Mungu.
Aleluya.
INJILI
Yn.
7:24 – 30
Wajumbe
wa Yohane walipokwisha ondoka, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za
Yohane, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitiswa na upepo? Lakini
mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mwororo? Jueni, watu wenye
mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme. Lakini,
mlitoka kwenda kuona nini? Nabii? Naam, nawambia, na aliye zaidi ya nabii. Huyo
ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako,
Atakayeitengeneza njia yako mbele yako.
Nami
nawaambia, Katika wale waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohane;
lakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye.
Na
watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa
wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohane. Lakini, Mafarisayo na wanasheria walilipinga
shauri la Mungu juu yao, kwa kuwa hawakubatizwa naye.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment