“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Desemba 2, 2021
Juma
la 1 la majilio
Isa.
26:1-6;
Zab
118:1,8-9,19-21,25-27;
Mt
7:21.24-27
NI
KITU GHANI KINATUFANYA TUSITIKISIKE?
Leo
tunasikia kuhusu wajenzi wawili, mmoja anafanikiwa kwa kujenga nyumba yake juu
ya mwamba, na mwingine anashindwa kwa kujenga nyumba yake juu ya mchanga.
Mjenzi wa kwanza anaweza kufananishwa na mfuasi wa Kristo ambaye hasikilizi tu
neno la Mungu nakuliacha bali analiishi na kulitenda. Kwa upande mwingine, yule
anaye sikia maneno ya Kristo, lakini hayaweki katika matendo ni kama yule
mjenzi wa pili aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga; kati yetu tumejenga
nyumba nzuri kwa mwamba mzuri ili kujilinda wenyewe na tufani mbali mbali,
lakini je! Tumeandaa mioyo yetu ili kumpokea Yesu wakati wa Noeli?
Ujumbe
wa Injili upo wazi: kama tunataka kushinda mawimbi na dhoruba za maisha na
kubaki tukiwa tumesimama imara, tunapaswa kuyaweka maneno ya Yesu ndani kabisa mwa
mioyo yetu na kuyaweka katika matendo yetu ya kila siku. Yesu ndiye mwamba
imara pekee ambao tunaweza kuwa na tumaini la kweli la kusimamia. Ni msingi wa
jinsi tulivyo na yote tunayo tumaini. Ni mwamba ambao Imani yetu imejengwa.
Njia pekee ya kumwilisha neno la Mungu katika maisha yetu, ni kusikia neno la
Mungu kila wakati katika akili yetu (kusoma neno la Mungu kila wakati). Ni
kushibishwa na Neno.
Kipindi
hiki cha majilio ni muda ambao tumepewa na kanisa ili tuzame katika msingi wa
maisha yetu ya kiroho kwa kusikiliza na kutenda. Tunapo sikiliza, tunapaswa
kutenda katika hali ya kumngojea Masiha azaliwe katika mioyo yetu. Kwa njia
hii, Noeli itasherekewa katika mioyo yetu ilio simama imara na katika nyumba
zetu.
Sala:
Bwana, ninaomba maisha yako ulioishi ya kibinadamu yawe msingi wa maisha yangu.
Ninaomba maisha yangu yajengwe ndani mwako wewe ambaye ni jiwe la msingi. Yesu,
nakuamini. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment