MASOMO
YA MISA DESEMBA 2, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 1 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
26:1-6
Siku
ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu;
ataamuru wokovu kuwa kuta na mamboma. Wekeni wazi malango yake, taifa lenye
haki, lishikalo kweli, uingie. Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea
katika Amani kamilifu, kwa kuwa tunakutumaini.
Mtumainini
Bwana sikuzote, maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele. Kwa kuwa amewashusha
wakaao juu, mji ule ulioinuka, aushusha, aushusha hata nchi, auleta hata
mavumbini. Mungu utaukanyaga chini, naam, miguu yao walio maskini, na hatua zao
walio wahitaji.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
118:1,8-9,19-21,25-27a (K) 26
(K)
Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.
Mshukuruni
Bwana kwa kuwa ni mwema
Kwa
maana fadhili zak eni za milele,
Ni
heri kumkimbilia Bwana,
Kuliko
kuwatumainia wanadamu,
Ni
heri kumkimbilia Bwana
Kuliko
kuwatumainia wakuu. (K)
Nifungulieni
malango ya haki,
Nitaingia
na kumshukuru Bwana.
Lango
hili ni la Bwana,
Wenye
haki ndio watakaoliingia.
Nitakushukuru
kwa maana umenijibu,
Nawe
umekuwa wokovu wangu. (K)
Ee
Bwana, utuokoe, twakusihi,
Na
abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana,
Tumewabarikia
toka nyumbani mwa Bwana.
Bwana
ndiye aliye Mungu,
Naye
ndiye aliyetupa nuru. (K)
SHANGILIO
Isa.
55:6
Aleluya,
aleluya,
Mtafuteni
Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni maadamu yu karibu.
Aleluya.
INJILI
Mt.
7:21,24-27
Siku
ili, Yesu akawaambia wafuasi wake: Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana,
atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba
yangu aliye mbinguni.
Basi
kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye
akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, mvua ikanyesha, mafuriko yakaja,
pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa
juu ya mwamba.
Na
kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu,
aliyejenga nyumba juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo
zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment