“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Desemba 22, 2021,
Juma
la 4 la Majilio
1
Sam 1: 24-28;
1
Sam 2: 1, 4-8;
Lk
1: 46-56
MSIFU
MUNGU KILA WAKATI!
Wimbo
wa Maria unapaswa kulinganishwa na ule wa Hanna (1 Sam 2: 1-10) na Zakaria (Lk
1: 68-79). Wimbo huu unafunua furaha ya moyo wa Mama wa Mungu. Anakiri mambo
makuu aliomtendea Mungu na anaelezea furaha yake ya ndani. Ni vizuri kuona
kwamba “moyo” wake na “roho” yake vinafuraha. Vinaelezea matendo yake na
matendo ya Mungu. Moyo wa Mama yetu mbarikiwa vinaelezea uwezo wake wa
kibinadamu katika akili yake, hisia na matamanio. Hivi ndivyo vinamfanya
binadamu. Na katika hali hiyo ya kibinadamu anatangaza ukuu wa Mungu. Kwa
maneno mengine, kwa akili yake aliweza kuhisi ukuu wa Mungu, na hivyo anachagua
kuutukuza na kuutangaza ukuu wa Mungu na anafanya hivyo kwa hisia zake zote.
Utu wake wote ulimezwa na ukuu wa Mungu.
Wakati
unabii wa Maria ukisimama katika hali mbalimbali, utofauti wake mkubwa ni
katika maana zake. Hanna anamsifu Mungu kwa kumtoa Samueli. Alikuwa katika aibu
ya kuwa mgumba (1 Sam 1: 7). Kuzaliwa kwa Samueli kumebadilisha yote hayo, na
ana sababu ya kumsifu Mungu. Kadhalika, Zakaria amevumilia kwa muda wa miaka
mingi bila kuwa na mtoto na kuwa bubu kwa miezi tisa (Lk 1: 20, 62). Na sasa
mtoto wake amezaliwa, na ulimi wake ukafunguliwa, (Lk 1: 64), na ana kila
sababu ya kumsifu Mungu. Kwa kulinganisha, tunaona Luka anaweka, sifa za Maria
mwanzoni kabisa mwa mimba yake. Alikuwa anamsifu Mungu sio baada tu ya mateso
lakini kabla na wakati wa mateso. Alikuwa akisifu katika hali zote. Alikuwa
akisifu kwa Imani na sio kwasababu ameona jambo fulani (2 Cor 5: 7).
Je,
mimi na wewe tunaiga huu mfano kamili wa Mama yetu mbarikiwa, kama alivyo
tafuta kufahamu, kupenda na kutangaza ukuu wa Mungu kwa mwili wake wote? Je,
unaruhusu roho Mtakatifu kufurisha moyo wako na furaha? Tuombee kwa ajili ya
neema ya Mungu “tutangaze” na “tufurahi” pamoja naye anapozaliwa Mwana wa
Mungu, ili wewe pia uweze kuimba wimbo wa furaha!
Sala:
Mama mpendwa, ulionesha mfano kamili wa jinsi ya kuishi kwa Imani na uaminifu
na unyenyekevu wa mtumishi wa Mungu aliye juu. Ulitangaza ukuu wake na ulijazwa
na furaha ya kuja kwake. Nisaidie mimi, kwa maombezi yako yenye nguvu, niweze
kuiga Imani yako, kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote. Mama Maria niombee mimi.
Yesu nakutumainia wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment