MASOMO
YA MISA, DESEMBA 22, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 4 LA MAJILIO
SOMO
1
1
Sam. 1:24 – 28
Siku
zile, hana alimchukua Samweli pamoja naye, na ng’ombe watatu, na efa moja ya
unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa Bwana, huko Shilo; na yule mtoto
alikuwa mtoto mdogo. Nao wakamchinja huyo ng’ombe, wakamleta mtoto kwa Eli.
Hana
akasema, Ee Bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule
mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba Bwana. Naliomba nipewe mtoto
huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa
Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu
Bwana huko.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
1
Sam. 2:1, 4 – 8 (K) 1
(K)
Moyo wangu wamshangilia Bwana Mwokozi wangu.
Moyo
wangu wamshangilia Bwana,
Pembe
yangu imetukuka katika Bwana.
Kinywa
changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa
kuwa naufurahia wokovu wako. (K)
Pinde
zao mashujaa zimevunjika,
Na
hao waliojikwa wamefungiwa nguvu.
Walioshiba
wamejikodisha ili kupata chakula,
Na
hao waliokuwa na njaa wamepata raha.
Naam,
huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba,
Na
yeye aliye na wana wengi amedhoofika. (K)
Bwana
huua, naye hufanya watu hai;
Hushusha
hata kuzimu, tena huleta juu.
Bwana
hufurahisha mtu, naye hutajirisha;
Hushuhsa
chini, tena huinua juu. (K)
Humwinua
mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha
mhitaji kutoka jaani,
Ili
awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi
kiti cha enzi cha utukufu. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Mfalme wa mataifa na jiwe la msingi wa Kanisa uje kumwokoa mwanadamu
aliyemuumba kwa udongo.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:46 – 56
Sik
ile Maria alisema: Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia
Mungu, Mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana,
tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa; kwa kuwa mwenye nguvu
amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata
vizazi kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; amewatawanya walio na
kiburi katiak mawazo ya mioyo yao; amewaangusha wakuu kati aviti vyao vya enzi;
na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, na wenye mali amewaondoa
mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; ili kukumbuka rehema zake;
kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Mariamu
akakaa naye kadiri ya miezi mitatu kisha akarudi kwenda nyumbani mwake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment