“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumma,
Desemba 24, 2021,
Juma
la 4 la Majilio
2
Sam 7: 1-5, 8-12, 14, 16;
Zab
88: 2-5, 27, 29;
Lk
1: 67-79
MATAMANIO YAKO YATAKATIFUZWE
Ndugu wapendwa, karibuni kwa tafakari ya neno la Mungu
asubuhi ya leo katika adhimisho la Misa Takatifu. Neno la Mungu leo katika somo
la kwanza, tunamsikia Mungu akimwahidia mfalme Daudi mambo makubwa kwamba moja
ya uzao wake atakuwa mfalme milele, na ndiye atakayeleta ahueni kwa Israeli.
Daudi
aliweza kuahidiwa hili kutokana na wazo lake jema, wazo la kutaka kumjengea
Bwana hekalu, alijitafakari na kuona aibu kwamba alikuwa akilala nyumba nzuri
kuliko nyumba ya Mungu na hivyo basi akaamua kusema atamjengea mwenyezi Mungu
hekalu.
Mungu
aliridhika na nia yake tu na kwa kweli aliishia kubarikiwa namna hii. Yeye
alikuwa mfalme wa kwanza kutamani kumjengea Mwenyezi Mungu nyumba na ikapelekea
kuahidiwa urithi wa kifalme uliodumu milele.
Hapa
tupate somo ndugu zangu. Kuna wakristo baadhi unakuta tunatoka nyumba nzuri
lakini wanasali kwenye kigango chenye nyasi. Wanatoka kwenye marumaru wanaenda
kusali kwenye makuti-au wanatokea kwenye makochi halafu wanaenda kukaa juu ya
mawe au majamvi. Na unakuta baadhi ya wakristo ni waseremala lakini hatujaribu
hata kutengeneza kabati au kiti cha kanisani. Na wanaridhika tu, wanakalia viti
vichafu. Hii ni kujinyima baraka. Au unakuta wewe unatoka nyumba safi halafu
unaenda kanisani kukaa sehemu chafu; unakuta wewe ni meneja wa benki au mhusika
usafi wa taasisi fulani lakini pale kanisani kwako ni pachafu kweli. Halafu
tunaridhika tu.
Nabii
Hagai anasema wengi wamelaaniwa kwa sababu wameitelekeza nyumba ya Bwana. Huyu
Daudi alipata kubarikiwa kwa kuijali nyumba ya Bwana. Sisi tusiitelekeze nyumba
ya Bwana. Au ukija kudeki kanisani, hudeki vizuri kama kule chumbani kwako,
unadeki tuu alimradi umalize.
Katika
somo la injili, tunakutana na unabii wa Zakaria. Anakiri kwamba Bwana hakika
haachi kutimiza ahadi zake. Ametupatia Mwokozi aliyemzao wa Daudi atakayekuja
kutukomboa.
Jana
tuliona kwamba nchi lazima ifunguke ili iweze kumpokea huyu Mwokozi,
isipofunguka, huyu Mwokozi anakuja tu na kupita. Wengi anakuja na kupita kwa
sababu mioyo yetu haijafunguka. Imefungwa na dhambi bado. Tuwe tayari tumpokee
Bwana wetu.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment