MASOMO
YA MISA,
IJUMMA,
24 DESEMBA 2021
JUMAMOSI
YA 4 YA MAJILIO
SOMO
1
2Sam.
7:1-5, 8-11, 16
Ikawa,
mfalme Daudi alipokuwa akikaa katika nyumba yake, hapo Bwana alipomstarehesha,
asiudhiwe na adui zake waliomzunguka pande zote, mfalme akamwambia Nathani,
nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa nyumba mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa
ndani ya mapazia. Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni
mwako; maana Bwana yu pamoja nawe.
Ikawa
usiku uo huo, neno la Bwana likamfikia Nathani kusema, Enenda, ukamwambie
mtumishi wangu, Daudi, Bwana asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae
ndani yake? Nalikutwa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo ili uwe
mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli; nami nimekuwa pamoja nawe kila
ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia
jina kuu, kama jina la wakuu walioko duniani. Tena nitawaagizia mahali watu
wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe
tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza; naam, kama vilivyokuwa
tangu siku ile nilipowaamuru waamuzi, wawe juu ya watu wangu Israeli; nami
nitakustarehesha mbele ya adui zako wote.
Tena
Bwana anakuambia ya kwamba Bwana atakujengea nyumba. Na nyumba yako, na ufalme
wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara
milele.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
89:1-4, 27, 29 (K) 1
(K)
Fadhili za Bwana nitaziimba milele.
Fadhili
za Bwana nitaziimba milele;
Kwa
kinywa change nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana
nimesema, fadhili zitajengwa milele;
Katika
mbingu utauthibitisha uaminifu wako. (K)
Nimefanya
agano na mteule wangu,
Nimemwapia
Daudi, mtumishi wangu.
Wazao
wako nitawafanya imara milele;
Nitakijenga
kiti chako cha enzi hata milele. (K)
Nami
nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza;
Kuwa
juu sana kuliko wafalme wa dunia.
Wazao
wake nao nitawadumisha milele,
Na
kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. (K)
SHANGILIO
Aleuya,
aleluya,
Ee
Utokaye Mashariki, Uliye mnga’ao wa mwanga wa milele na jua la haki, Njoo
kuwaangazia wakaao gizani na katika kivuli cha mauti.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:67-79
Siku
ile, Zakaria, baba yake Yohane alijazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akisema,
Atukuzwe
Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.
Ametusimamishia pembe ya wokovu katika mlango wa Daudi, mtumishi wake. Kama
alivyosema tangu mwanzo kwa kinywa cha manabii wake watakatifu; tuokolewe na
adui zetu na mikononi mwao wote wanaotuchukia; ili kuwatendea rehema baba zetu,
na kulikumbuka agano lake takatifu; uapo aliomwambpia Ibrahimu, baba yetu, ya
kwamba atatujalia sisi, tuokoke mikononi mwa adui zetu, na kumwabudu pasipo
hofu, kwa utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote.
Nawe,
mtoto, utaitwa nabii wake aliye juu, kwa maana utatangulia mbele za uso wa
Bwana umemtengenezea njia zake; uwajulishe watu wake wokovu, katika kusamehewa
dhambi zao. Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, ambazo kwa hizo mwangaza utokao
juu umetufikia, kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, na kuiongoza
miguu yetu kwenye njia ya Amani.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment