MASOMO
YA MISA DESEMBA 8, 2021
JUMATANO
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SHEREHE
YA BIKIRA MARIA MTAKATIFU, MKINGIWA DHAMBI YA ASILI
SOMO
1
Mwa.
3:9-15,20
Adamu
alipokwisha kula matunda ya mti, Bwana Mungu alimwita, akamwambia Uko wapi?
Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, naliogopa kwa kuwa mimi ni uchi;
nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe
matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa
awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Bwana
Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka
alinidanganya, nikala.
Bwana
Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko
wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na
mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe
utamponda kisigino.
Adamu
akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio
hai.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
98:1-4 (K) 1
(K)
Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Kwa
maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono
wa kuume wake mwenyewe,
Mkono
wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)
Bwana
ameufunua wokovu wake,
Machoni
pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka
rehema zake,
Na
uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)
Miisho
yote ya dunia imeuona,
Wokovu
wa Mungu wetu.
Mshangilieni
Bwana, nchi yote,
Inueni
sauti, imbeni kwa furaha. (K)
SOMO
2
Efe.
1:3-6, 11-12
Atukuzwe
Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni,
katika ulimwengu war oho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika
yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na
hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe
wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na Uradhi wa mapenzi yake. Na usifiwe
utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Na ndani yake
sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi
lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Nasi katika
huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi tuliotangulia kumwekea Kristo
tumaini letu.
SHANGILIO
Lk.
1:28
Aleluya,
aleluya,
Salamu,
Mariamu, ulipewa neema. Bwana yu pamoja nawe! Umebarikiwa katika wanawake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:26-38
Malaika
Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya
Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema,
Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili
ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika
akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. Tazama, utachukua
mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo atakuwa mkuu,
ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba
yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna
mwisho.
Mariamu
akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana hujui mume? Malaika akajibu
akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu
zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa
kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua
mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye
aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.
Mariamu
akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha
malaika akaondoka akaenda zake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment