“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Desemba 8, 2021,
Juma
la 2 la Majilio
Sherehe
ya Bikira Maria Mtakatifu Mkingiwa dhambi wa Asili
Mwa
3:9-15, 20;
Zab
97:1-4;
Efe
1:3-6,11-12;
Lk
1:26-38
BWANA
AMENITENDEA MAMBO MAKUU, JINA LAKE NI TAKATIFU.
Kila
mtu amezaliwa na dhambi kwasababu ya kushiriki katika dhambi ya Adamu. Lakini
katika sehemu zote za maisha kuna neno liitwalo “Upekee”. Hivyo upekee
ulitolewa kwa Maria kwasababu alichaguliwa na Bwana kuwa Mama wa Mwanae. Maria
hakuzaliwa na hali ya dhambi kama tunayozaliwa nayo sisi. Alikuja ulimwenguni
akiwa na uhalisia kamili wa ubinadamu kama ule wa Hawa na Adamu kabla ya
kutenda dhambi na kuanguka mbali na neema. Mungu alimpa Maria hali hii kamili
ya asili ya ubinadamu sio kwa sababu Maria alifanya kitu kikuu bali kwasababu
alikuwa akienda kutenda kitu kikuu. Hivyo wakati wa kupokea kwake mimba
kulikuwa ni neema maalumu kutoka kwa Mungu, kisha tokea hapo lilikuwa ni jukumu
lake kubakia msafi na bila doa lolote. Hili alilifanya. Sisi sote tumeitwa
“kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na
hatia mbele zake katika pendo.” (Efe 1:4).
Utakatifu
wa Maria ni matokeo ya neema ya Mungu na utayari wake wa kuwa wazi kwa neema
hiyo. Kutokupata dhambi ya asili ni kwasababu ya neema ya Mungu kupitia kwa
Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo. Kwahiyo Maria kukingiwa dhambi ya asili sio
namna ya kumpa heshima kwa njia yake mwenyewe bali kwa njia ya Mwanae Yesu
Kristo. Kristo kutokuwa na dhambi ni kwasababu ya yeye kuwa nafsi ya pili ya
Mungu. Na Maria kutokuwa na dhambi ni kwasababu ya neema ya Mungu pekee na
kushirikiana kwake na neema hiyo. Kanisa la kwanza walimheshimu Bikira Maria
kwa namna ya pekee kati ya watakatifu wote, kwasababu ya kushiriki kwake katika
fumbo la umwilisho wa Mwanae Yesu Kristo na kwasababu ya neema iliotoka katika
kushiriki kwake katika fumbo hili.
Neema
hiyo hiyo inatolewa kwetu sisi ili tuwe wasafi kupitia damu ya Kristo aliyekufa
kwa ajili yetu sisi, lakini je, tumejitoa kama Maria ili tuuishi vema wito
wetu?
Sala:
Bwana tufanye tuwe wasafi ndani ya mawazo, maneno na matendo yetu. Nisaidie
niweze kujenga maisha ya utukufu Mbinguni kwa njia ya kujikabidhi kwenye neema
yako. Yesu nakuamini wewe Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment