MASOMO
YA MISA DESEMBA 6, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
35:1-10
Nyika
na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama
waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba;
litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa
Bwana, ukuu wa Mungu wetu.
Itieni
nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. Waambieni walio
na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi,
na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.
Ndipo
macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu
aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana
katika maji yatabubujika; na vijito jangwani.
Na
mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa
chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na
majani, pamoja na mianzi na manyasi.
Na
hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi
hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa
wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama
mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda
katika njia hiyo.
Na
hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya
milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na
kuugua zitamkimbia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
85:8-13 (K) Isa. 35:4
(K)
Tazama Mungu wetu atakuja na atatuokoa.
Nisikie
atakavyosema Mungu Bwana,
Maana
atawaambia watu wake Amani.
Naam,
na watauwa wake pia,
Bali
wasiurudie upumbavu tena.
Hakika
wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu
ukae katika nchi yetu. (K)
Fadhili
na kweli zimekutana,
Haki
na Amani zimebusiana.
Kweli
imechipuka katika nchi,
Haki
imechungulia kutoka mbinguni. (K)
Naam,
Bwana atatoa kilicho chema,
Na
nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki
itakwenda mbele zake,
Nayo
itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Tazama
Mfalme, Bwana wa ulimwengu, Yeye ataiondoa nira ya utumwa wetu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
5:17-26
Ikawa
siku zile, Yesu alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati
walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi,
na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.
Na
tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu wmenye kupooza; wakataka
kumpeleka ndani na kumweka mbele yake. Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka
ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampitisha
katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya
Yesu. Naye alipoiona Imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Basi,
wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye
maneno ya kukufuru? N’nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?
Na Yesu alijua hoja zao, akajibu akawaambia, Mnahojiana nini mioyoni mwenu?
Lililo jepesi ni lipi? Kusema, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka,
uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya
kusamehe dhambi, (alimwmbia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitike
kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako. Mara hiyo akasimama mbele yao,
akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani mwake, huku akimtukuza
Mungu.
Ushaangao
ukawashika wote, wakamtukuza Mungu; wakajaa hofu, wakisema, Leo tumeona mambo
ya ajabu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment