“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu,
Desemba 6, 2021
Juma
la 2 la Majilio
Isa
35:1-10
Zab
85: 9-14
Lk
5: 17-26
JE
UNATAMANI KUPONYWA?
Katika
Injili ya leo, tunamwona Masiha akitimiza yale yale aliotabiri nabii Isaya
katika somo la kwanza leo, akitoa matumani mapya kwa wagonjwa na kuwaponya na
kuwafanya warukeruke tena kwa furaha. Katika Injili tunaona uponyaji wa mtu
aliyepooza katika hali ya Imani ya hali ya juu. Huyu mgonjwa hakuwa anajiweza
na alihitaji msaada wa kubebwa na mkeka na kuletwa kwa Yesu. Hawa marafiki
walipata vipingamizi kabla ya kumfikisha kwa Yesu kwa msaada. Kulikuwa na hali
ya kukatisha tamaa walipofika katika nyumba ile, lakini hawakukata tamaa.
Wanapanda juu ya paa, na kuondoa paa na kumshusha alipokuwa Yesu. Injili
inaeleza wazi kwamba ‘Yesu baada ya kuona Imani yao’. Huyu mgonjwa hakumtafuta
Yesu mwenyewe, Imani yake kwa Bwana ilisaidiwa na imani ya wenzake. Umoja wao
ulifanikisha. Yesu anamponya huyu mgonjwa na anamsamehe dhambi zake. Hapokei
uponyaji tu wa mwili bali uponyaji mkamilifu wa kuondolewa dhambi zake zote.
Tutafakari
leo juu ya hamu yetu ya kupokea Msamaha wa Mungu katika maisha yetu. Je,
unatamani kupokea huruma ya Yesu na msamaha wake katika maisha yako? Sababu ya
Yesu kuja ulimwenguni kutoka mbinguni ni kutusamehe dhambi zetu na
kutupatanisha na Mungu Baba. Miujiza mikubwa sio kigezo, kigezo ni msahama.
Utakapo pokea zawadi hii ya huruma na msamaha, utamtukuza pia Mungu kwa furaha.
Tunaomba kipindi hiki cha majilio kilete furaha mpya katika maisha yetu kwa
msamaha wa Mungu.
Sala:
Bwana, natamani huruma na msamaha katika maisha yangu. Nisaidie Bwana
nijishushe mbele yako ili niweze kusikia ukisema ‘dhambi zako zimesamehewa’.
Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment