MASOMO
YA MISA DESEMBA 4, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 1 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
30:19-21, 23-26
Bwana
Mungu Mtakatifu wa Israeli asema; watu watakaa katika Sayuni huko Yerusalemu;
wewe hutalia tena; hakika yake atakuonea rehema nyingi kwa sauti ya kilio
chako; asikiapo ndipo atakapokujibu.
Na
ingawa Bwana atawapeni chakula cha shida na maji ya msiba, lakini waalimu wako
hawatafichwa tena, ila macho yako yatawaona waalimu wako; na masikio yako
yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda
mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.
Naye
atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya
nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ngo’ombe zako watakula
katika malisho mapana. Ng’ombe pia na wanapunda wailimao nchi watakula chakula
kilichokolea, kilichopepetwa kwa ungo na kwa pepeo.
Na
juu ya kila mlima mrefu, na juu ya kila kilima kilichoinuka, itakuwapo mito na
vijito vya maji, katika siku ya machinjio makuu itakapoanguka minara. Na tena
nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba,
kama nuru ya siku saba, katika siku ile Bwana atakapofunga mapigo ya watu wake,
na kuliponya pigo la jeraha yao.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
147:1-6 (K) Isa. 30:18
(K)
Heri wote wamngojao Bwana.
Msifuni
Bwana, maana ni vema kumwimbia Mungu wetu,
Maana
kwapendeza, kusifu ni kuzuri.
Bwana
ndiye aijengaye Yerusalem,
Huwakusanya
waliotawanyika wa Israeli. (K)
Huwaponya
waliopondeka moyo,
Na
kuziganga jeraha zao.
Huihesabu
idadi ya nyota,
Huzipa
zote majina. (K)
Bwana
wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu.
Akili
zake hazina mpaka,
Bwana
huwategemeza wenye upole,
Huwaangusha
chini wenye jeuri. (K)
SHANGILIO
Isa.
33:22
Aleluya,
aleluya.
Bwana
ndiye mwamuzi wetu; Bwana ndiye mfanya sheria wetu; Bwana ndiye mfalme wetu;
Ndiye atakayetuokoa.
Aleluya.
INJILI
Mt.
9:35-10:1, 6-8
Siku
ile: Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika
masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, na kuponya magonjwa yote
na udhaifu wa kila aina.
Na
alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika
kama kondoo wasio na mchungaji. Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni
mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apelike
watenda kazi katika mavuno yake.
Akawaita
wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na
kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Akawaambia,
afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Na
katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia. Pozeni
wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni
bure.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment