MASOMO
YA MISA DESEMBA 25, 2021
SHEREHE
YA KUZALIWA BWANA
SOMO
1
Isa.
52:7-10
Jinsi
ilivyo mizuri juu ya milima, miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye
Amani, aletaye habari njema ya mambo mema, yeye atangazaye wokovu, auambiaye
Sayuni, Mungu wako anamiliki! Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao,
wanaimba pamoja; maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwan arejeavyo Sayuni.
Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa
ukiwa; Kwa kuwa Bwan amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu. Bwana
ameweka wazi mkono wake mtakatifu machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za
dunia zitauona wokovu wa Mungu wetu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
98:1-6 (K) 3
(K)
Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Kwa
maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono
wa kuume wake mwenyewe,
Mkono
wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)
Bwana
ameufunua wokovu wake,
Machoni
pa mataifa amedhihirisha haki yake,
Amezikumbuka
rehema zake,
Na
uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)
Miisho
yote ya dunia imeuona,
Wokovu
wa Mungu wetu,
Mshangilieni
Bwana nchi yote,
Inueni
sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. (K)
Mwimbieni
Bwana zaburi kwa kinubi,
Kwa
kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa
panda na sauti ya baragumu,
Shangilieni
mbele za Mfalme, Bwana. (K)
SOMO
2
Ebr.
1:1 – 6
Mungu,
ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia
nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa
mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa
utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake,
akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri ya jina alilorithi lilivyo tukufu
kuliko lao.
Kwa
maana alimwambia malaika yupi wakati wowote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo
nimekuzaa? Na tena, mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika
wote wa Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya!
Siku
takatifu imetung’aria: enyi mataifa njoni mkamwabudu Bwana, kwa sababu leo
mwanga mkubwa umeshuka duniani.
Aleluluya.
INJILI
Yn.
1:1-18
Hapo
mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye
hakikufanyika chochote kilichofanyika. Ndani yake ndimo ulikuwa uzima, nao ule
uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
Palitokea
mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohane. Huyo alikuja kwa ushuhuda,
ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru,
bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
Kulikuwako
Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. Alikuwako
ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu
haukumtambua. Alikuja kwake, wala wali wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale walioaminio jina lake;
waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya
mtu, bali kwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona
utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na
kweli.
Yohani
alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema. Huyu ndiye niliyenena habari zake ya
kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa
kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa
Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wao wote; Mungu Mwana pekee aliye
katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment