“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
25, 2021,
SHEREHE
YA KUZALIWA BWANA
Isa
52: 7-10;
Zab
98: 1-6;
Ebr
1:1-6;
Yn
1: 1-18
HURUMA
IMEPATA KUWA HAI!
Huruma
imepata kuwa hai na yenye kuonekana katika Yesu Mnazareti, na hata ikafikia
kilele chake katika Yeye. Baba “aliye mwingi wa rehema” (Efe 2:4), baada ya
kumfunulia Musa jina lake kuwa ni “Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si
mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli” (Kut 34:6), hakuwahi kuacha hata
mara moja kuonyesha hali yake ya kimungu katika nafasi zote za historia.
“Ulipowadia utimilifu wa wakati” (Gal 4:4), kila kitu kilipokuwa kimepangwa
kadiri ya utaratibu wake wa ukombozi, alimtuma duniani Mwanae pekee ili
kutufunulia upendo wake katika ukamilifu wake.
Huruma
ni chemchemi ya furaha, ya utulivu na ya amani. Ni sharti la wokovu wetu.
Huruma ni tendo la juu na kuu kabisa ambalo kwa njia yake Mungu anatujia sisi.
Huruma ni njia inayowaunganisha Mungu na binadamu, na kuufungulia moyo mlango wa
matumaini ya kupendwa daima, licha ya hali yetu ya dhambi. (Rej. BULA YA
KUZINDUA JUBILEI YA PEKEE YA HURUMA 1,2)
Leo
Kanisa pamoja na viumbe vyote vyajawa na furaha kwani vimefanywa upya na kuwa
kiumbe kipya kwa njia ya kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. “Neno” basi na
uwe mwanga (Mwa. 1:3), lililoleta uumbaji sasa limeongelewa tena, kupitia
kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mkombozi wetu. Mwanga (Yn. 1:8), sasa anang’ara
katika giza. Mwanga, atoaye mwanga kwa kila mtu amekuja ulimwenguni. Mungu
asiyefahamika, sasa amefanywa afahamike, Baba sasa anajidhihirisha mwenyewe,
kupitia mwanae wa kiume, Yesu. Neno alifanyika mwili na akakaa kwetu.
Umwilisho
au Noeli ni sherehekeo la furaha hii – Mungu wetu anakuwa mwili na anakuja
kukaa ndani yetu wanadamu. Tukio hili liliufanya ulimwengu ufurahi , malaika
walifurahi kwa Utukufu kwa Mungu, waliomba kwaajili ya amani duniani kwa watu.
Ingawa ukaribisho wa Bwana Yesu haukuwa wa furaha sana ulimwenguni. Mkombozi
hakuwa na nafasi ya kuzaliwa, bali katika uhakika, katika moja ya vijiji vidogo
Bethlehemu. Hakuwa na tafrija ya ukaribisho, isipokuwa tu kwa baadhi ya wanyama
katika hali ya ukimya na baadae wachungaji wachache waliomuabudu Yeye. Mfalme
Herode alimchukulia mtoto kuwa kama ni tishio, alitaka mtoto Yesu auwawe. Katika
miaka ya mbeleni, mkombozi wetu alikanwa, alivamiwa na kusulubiwa. Na kwa hayo
yote aliyoyapokea, mkombozi pekee alirudisha huruma, huruma na upendo. Leo,
Yesu amezaliwa kati yetu tena, katika hali yetu ya kumkana na hali ya dhambi;
Yeye amezaliwa Bethlehemu ya hali ya ubinafsi, umimi, mateso, vita, unyonyaji,
nakadhalika. Je, sisi tupo kama wachungaji, waliokwenda kwa Yesu na kuzitoa
heshima zao au tupo kama Herode, aliyemchukua Yesu kuwa kama ni tishio la uhuru
wetu, katika hangaiko la kutafuta starehe?
Je, tunakwenda kufurahi pamoja na wachungaji au kupanga mabaya kama
Herode?
Katika
milongo miwili iliyopita, dunia yetu imekuwa nzuri sana kwa wanadamu pamoja na
uwepo wa kimungu wa Mungu mwenyewe. Ndani yake pia, wengi wametamani kuwa
katika giza. Kwa namna ya pekee, Yesu anahitaji azaliwe ndani yetu, awe Neno
liletalo, mwanga unaoondoa giza lote, huruma inayo futa dhambi zetu. Je, tupo
tayari kujitoa wenyewe kwake Yeye? Je, tupo tayari kuufahamu mwanga huo? Je,
tupo tayari kupokea huruma yake?
Sala:
Bwana Yesu, nakuhitaji Wewe uzaliwe ndani yangu leo, Nahitaji huruma yako
inifanye chombo kikamilifu kwako. Ninahitaji kunena juu yako katika maneno na
maisha yangu. Amina.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment