MASOMO
YA MISA, DESEMBA 23, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
Mal.
3:1 – 4; 4:5 – 6
Bwana
Mungu asema: Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele
yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule
mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.
Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Kwa maana yeye ni mfano wa
moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye
ataketi kama asafishaye fkama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa
wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolewa Bwana dhabihu
katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele
za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.
Angalieni,
nitawapelekea Eliya nabii, kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na
kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto
iwaelekee baba zao, ioli nisije nikaipiga dunia kwa laana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
25:4 – 5, 8 – 10, 14
(K)
Changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.
Ee
Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe
mapito yako.
Uniongoze
katika kweli yako,
Na
kunifundisha.
Maana
wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu. (K)
Bwana
yu mwema, mwenye adili,
Kwa
hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
Wenye
upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye
upole atawafundisha njia yake. (K)
Njia
zote za Bwana ni fadhili na kweli,
Kwao
walishikao agano lake na shuhuda zake.
Siri
ya Bwana iko kwao wamchao,
Naye
atawajulisha agano lake. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Imanueli, Mfalme na Mwanasheria wetu, njoo ukatuokoe, ee Bwana, Mungu wetu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:57 – 66
Ikawa,
siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia
jirani zake na jamaa zake, wakafurahi pamoja naye.
Ikawa
siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria.
Mamayeakajibu akasema, La, sivyo; bali, ataitwa Yohani. Wakamwambia, Hapana mtu
katika jamaa zake aitwaye jina hilo. Wakamwashiria babaye wajue atakavyo
kumwita. Akataka kibao, akaandika kwamba, Jina lake ni yohane. Wakastaajabu
wote. Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena
akimsifu Mungu.
Wakaingiwa
na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa
katika nchi yote ya milima milima ya Uyahudi. Na wote walioyasikia wakayaweka
mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa wa namna gani. Kwa sababu mkono wa
Bwana ulikuwa pamoja naye.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment