“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Desemba 23, 2021,
Juma
la 4 la Majilio
Mal
3: 1-4, 23-24;
Zab
24: 4-5, 8-10, 14;
Lk
1: 57-66
KURUDI
KWA BWANA!
Ama
kweli Yesu ni mkuu. Nabii Malaki katika somo la kwanza anatabiri ujio wa mjumbe
kuandaa siku ya ujio wake. Inaonesha kwamba dunia ilijiandaa kwa ujio mkubwa;
ujio wa Mungu duniani. Hivyo, iliwabidi watu watubu na kujitakasa ili waupatie
heshima uwepo wa Mungu duniani. Dhambi humkufuru Mungu.
Nabii
Malaki anatangaza ujio wa mjumbe, Elia kuandaa ujio huo. Sasa katika injili,
mjumbe huyu anazaliwa, na Malaika Gabrieli alimweleza Zakaria kwamba Roho na
nguvu ya Elia itakuwa juu yake (Lk 1:17). Huyu ndiye atakayewaandaa watu kwa
ujio wa Masiha. Yohane alifanya kazi hii kwa uaminifu. Alihubiri na kuwahimiza
watu waache dhambi na kubatizwa ubatizo wa toba. Pia alimtambulisha Masiha
alipofika. Lakini baadhi walikataa kutubu na kumpokea kama Masiha. Lakini Yesu
alivumilia kukaa nao, akavumilia kufuru walizomfanyia. Kweli Yesu alikuwa na
huruma sana. Sisi tusiwe kama hawa. Tunapokaribia kuadhimisha kumbukumbu ya
kuzaliwa kwake, tumpatie Kristo heshima yake kwa kuziungama dhambi zetu. Pia
tuepuke kupokea Ekaristi katika hali ya dhambi.
Tukisha
ungama anataka tubaki naye katika hali ya usafi. Yesu aliwaambia wanafunzi wake
“Salini msije mkaingia katika vishawishi” (Lk 22: 46). Kwa namna nyingine Sala
inamsaidia Mkristo kutokuingia kwenye dhambi au sala ni silaha ya kujikinga
dhidi ya muovu. Tunaweza kujiuliza mbona nina Sali lakini ninaanguka kwenye
dhambi daima? Wengi wetu hatusali vizuri. Pengine tunasali ili watu watuone
watusifu kwamba tunasali sana, wengine tunasali kwasababu tunaogopa kutengwa na
jumuiya, wengine tunasali ili kutishia watu watuogope, wengine tunasali watu
watuheshimu, wengine tunasali ili watu wakiniona nasali siku ikitokea wanipe
nafasi ya kwanza kwasababu wataona nina Mungu ndani yangu.
Aina
hizo za sala, shetani akija atakubeba vizuri kama upepo. Sali kwa Baba katika
hali ya ndani ya kweli mpe yeye utukufu na heshima yote irudi kwa kwake, na
daima jiunge naye katika hali hii, nakwambia hapa maneno ya Yesu yatafanya kazi
kweli “kwamba salini ili msiingie katika vishawishi”, hutarudi tena kwenye
dhambi kirahisi. Pekee yetu hatuwezi tunahitaji msaada wa Mungu, tumwombe atupe
nguvu ili Mwanae azaliwe katika hali ya neema katika roho zetu.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment