MASOMO
YA MISA, DESEMBA 21, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
Wimb.
2:8 – 14
Sikiliza!
Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja akiruka milimani, akichachawa vilimani.
Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu,
achungulia dirishani, atazama kimiani.
Mpendwa
wangu alinena, akaniambia, ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, maana
tazama, kaskazi imepita, masika imekwisha, imekwenda zake; maua yatokea katika
nchi, wakati wa kupelea umefika, na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. Mtini
wapevusha tini zake, na mizabibu inachanua inatoa harufu yake nzuri.
Ondoka,
mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako. Hua wangu, mafichoni mwa jabali, katika
sitara za magenge, nitazame uso wako, nisikie sauti yako, maana sauti yako ni
tamu na uso wako mzuri.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
Au.
Sef.
3:14:14 – 17
Imba,
ee binti Sayuni; piga kelele, ee Israeli; furahi na kushangilia kwa moyo wako
wote, ee binti Yerusalemu. Bwana ameziondoa hukumu zako, amemtupa nje adui
yako; mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana, yu katikati yako; hutaogopa uovu
tena.
Katika
siku ile Yerusalemu utaambiwa, usiogope, ee Sayuni; mikono yako isilegee.
Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa
furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
33:2 – 3, 11 – 12, 20 – 21 (K) 1, 3
(K)
Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki: Mwimbieni wimbo mpya.
Mshukuruni
Bwana kwa kinubi,
Kwa
kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
Mwimbieni
wimbo mpya,
Pigeni
kwa ustadi kwa sauti ya shangwe. (K)
Shauri
la Bwana lasimama milele,
Makusudi
ya moyo wake vizazi na vizazi.
Heri
taifa ambalo Bwana ni Mungu wako,
Watu
aliowachagua kuwa urithi wake. (K)
Nafsi
zetu zinamngoja Bwana;
Yeye
ndiye msaada wetu na ngao yetu.
Maana
mioyo yetu itamfurahia,
Kwa
kuwa tumelitumaini jina lake takatifu. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
Utokaye Mashariki, uliye mng’ao wa mwanga wa milelel na jua la haki, njoo
kuwaangazia wakaao gizani na katika kivuli cha mauti.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:39 – 45
Mariamu
aliondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja
wa Yuda, akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti
aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo
lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema,
Umebarikiwa
wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno
hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako
ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya
tumbo langu. Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment