“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumanne,
Desemba 21, 2021,
Juma
la 4 la Majilio
Wimb
2: 8-14;
Zab
33:2-3, 11-12, 20-21;
Lk
1: 39-45.
MAISHA
YETU WIMBO WA FURAHA
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu
asubuhi ya leo. Leo basi mada yetu kuu tunayojifunza ni kwamba Yesu ni sababu
ya furaha; ujio wake ni furaha. Mama Maria anayembeba Yesu alipofika kwa
Elisabeth, Elisabethi alifurahi kabisa, matatizo yake yaliyokuwa yakimwandama
kwa kuwa na mimba aliyasahau na kushangilia. Na hata kitoto kilichokuwa ndani
ya tumbo lake kilishangilia kwa furaha.
Somo
la kwanza linatumia pichaa ya mpendwa anayetembea juu ya milima akija kutangaza
furaha. Huyu mpendwa ni Yesu na leo inadhihirika jinsi anavyokuwa sababu ya
Elisabethi kufurahi. Kama alikuwa sababu ya Elisabethi kufurahi, hakika atakuwa
sababu yetu kufurahi pia, hakika tukimuamini hatatuacha katika hali ya kukosa
imani na kukata tamaa na matumaini.
Hakika
Yesu anapaswa kuwa sababu ya sisi kufurahi, tunapaswa kuangalia ni kipi
kinachotufanya Yesu asipate kuwa sababu ya sisi kufurahi na kubakia katika
huzuni. Kikubwa ni tamaa, kutokuridhika na kile nilichonacho na kutojiamini na
kile nilichopewa na Bwana.
Kutoridhika
na kile tulichopewa na Bwana kimetufanya tuwe watu wa kuwaangalia wengine tu,
tukitamani vya kwao na kusahau kukuza kipaji tulichopewa na Bwana na ndio
sababu wengi wetu ni maskini. Basi tusikubali Yesu apite kwetu kila siku na
sisi kushindwa kupata furaha kama Elisabethi-lazima tujiulize ni kitu gani
hicho kinanizuia?
Maria
alimpeleka Yesu kwa Elisabethi na hapa Elisabethi alipata kufurahi. Sisi
tujifunze kuwapelekea wenzetu Yesu, yaani habari njema. Hata kama tunaoujumbe
wa kuonya au kukaripia wenzetu, lazima tujifunze namna ya kuwaeleza ili basi
nao wafarijike, mara nyingi tumetumia lugha au mazingira mabaya na ndio maana
tumeishia kuwaletea wenzetu machungu makubwa.
Sisi
tuwe kama Maria, tukifika kwa wenzetu wafurahi. Pia kipindi hiki tuwakumbuke
pia mayatima, tuwapelekee Yesu, tuwachangie kitu, ni namna ya kuwaeleza kwamba
Kristo ni wetu sote; basi tufurahi.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment