MASOMO
YA MISA, DESEMBA 20, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 3 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
7:10 – 14
Siku
zile, Bwana alisema na Ahazi akinena, Jitakie ishara ya Bwana, Mungu wako;
itake katika mahali palipo chini sana, au katika mahali palipo juu sana. Lakini
Ahazi akasema, Sitaitaka, wala sitamjaribu Bwana. Naye akasema, Sikilizeni
sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata
mkataka kumchosha Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara.
Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake
Imanueli.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
24:1 – 6 (K) 7
(K)
Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Nchi
na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia
na wote wakaao ndani yake.
Maana
ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na
juu ya mito ya maji aliithibitisha. (K)
Ni
nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni
nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu
aliye na mikono safi na moyo mweupe.
Asiyeiinua
nafsi yake kwa ubatili. (K)
Atapokea
Baraka kwa Bwana,
Na
haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki
ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao
uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Ee
ufunguo wa Daudi, ufunguaye milango ya ufalme wa milele, njoo kuwaokoa watu
wako waliofungwa katika gereza la giza.
Aleluya.
INJILI
Lk.
1:26 – 38
Malaika
Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa
mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya
Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Akaingia
nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema. Bwana yu pamoja nawe. Naye
akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya
namna gani?
Malaika
akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepta neem akwa Mungu. Tazama,
utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. Huyo
atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi
cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake
utakuwa hauna mwisho.
Mariamu
akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu
akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu
zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa
kitakatifu, Mwana wa Mungu. Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua
mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye
aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.
Mariamu
akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha
malaika akaondoka akaenda zake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment