MASOMO
YA MISA DESEMBA 11, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
SOMO
1
Ybs.
48:1-4,9-11
Ndipo
aliposimama Nabii Eliya, kama moto, hata na neno lake likawaka kama tanuru.
Yeye alileta taa juu yao, na kwa juhudi yake akawapunguzia hesabu yao; kwa neno
la Bwana akazifungu mbingu, na mara tatu kutoka huko akateremsha moto. Jinsi
unavyotisha kwa miujiza yako! Aliye mfano wako aona fahari.
Ukachukuliwa
juu katika kisulisuli, katika gari la farasi wa moto. Ukaandikiwa kuwa utaleta
makemeo, ili kutuliza hasira siku ile ya Bwana; kugeuza moyo wa baba umwelekee
mwana na kuhuisha kabila za Israeli.
Bila
shaka wamebarikiwa wale waliokuona kwa macho, wakafa; lakini wewe umezidi
kubarikiwa, kwa maana unaishi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
80:1-2,14-15,17-18 (K) 3
(K)
Ee Bwana Mungu wetu, uturudishe, Utuangazishe uso wako, nasi tutaokoka.
Wewe
uchungaye Israeli, usikie,
Wewe
umwongozaye Yusufu kama kundi;
Wewe
uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Mbele
ya Efraimu, na Benyamini, na Manase,
Uziamshe
nguvu zako,
Uje,
utuokoe. (K)
Ee
Mungu wa majeshi, tunakusihi, urudi,
Utazame
toka juu uone, uujilie mzabibu huu.
Na
mche ule ulioupanda.
Kwa
mkono wako wa kuume;
Na
tawi lile ulilolifanya,
Kuwa
imara kwa nafsi yako. (K)
Mkono
wako na uwe juu yake,
Mtu
wa mkono wako wa kuume;
Juu
ya mwanadamu uliyemfanya,
Kuwa
imara kwa nafsi yako;
Basi
hatutakuacha kwa kurudi nyuma;
Utuhuishe
nasi tutaliitia jina lako. (K)
SHANGILIO
Lk.
3:4,6
Aleluya,
aleluya,
Itengenezeni
njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake,
Na
wote wenye mwili watauona wokovu wa Mungu,
Aleluya.
INJILI
Mt.
17:10-13
Walipokuwa
wakishuka kutoka mlimani, wanafunzi wake wakamwuliza Yesu wakisema: Kwa nini
waandishi hunena ya kwamba imempasa Eliya kuja kwanza?
Naye
akajibu, akawaambia, Kweli Eliya yuaja kwanza, naye atatengeneza yote; ila
nawaambia ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, lakini wakamtenda yote
waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu naye yuaenda kuteswa kwao.
Ndipo
wale wanafunzi walipofahamu ya kuwa amesema nao habari za Yohana Mbatizaji.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment