“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Desemba 11, 2021
Juma
la 2 la Majilio
YbS
48: 1-4, 9-11;
Zab
79: 2-3, 15-16, 18-19;
Mt
17: 10-13
KUKUBALI
KUTUBU
Kazi
ya Yohane Mbatizaji kama Elisha aliyekuja Waandishi walishindwa kuiona.
Walishindwa kumuona yeye akitimiza kazi ya Elisha ya kuandaa njia kwa ajili ya
Bwana. Kama Yohane alivyokuwa na kazi ya pekee ya kumtambulisha na kuandaa njia
kwa ajili ya ujio wa Kristo, sisi pia tuna kazi ya kumkaribisha Yesu daima.
Yesu alikuja miaka mingi iliopita, lakini daima anatamani kuja daima katika
maisha yetu. Na anaweza kuja tu kama tumejiandaa vizuri.
Ujumbe
mkuu wa Yohane ni kutubu dhambi zetu. Ingawaje sisi wote tunakazana kujikinga
na dhambi, kwasababu ya matokeo ya kuanguka kwa Mwanadamu, hatupaswi kusahau
kwamba wito wetu ni kuwa wakamilifu, kuwa wakamilifu kama Baba yetu wa Mbinguni
alivyo mkamilifu. Tunaitwa kutambua dhambi zetu, kuziungama, na kujitahidi
kujinasua kutoka kwenye dhambi hizo.
Kipindi
cha majilio ni kipindi muhimu cha kufanya hivyo daima, na ni muhimu kutafuta
neema zinazopatikana kwa neema ya Sakramenti ya kitubio katika kipindi hiki
kitakatifu. Tujitazame wenyewe katika mioyo yetu ni kwa jinsi ghani tulivyo
tayari kuihubiria mioyo yetu kuhusu kutubu na kuacha dhambi. Kukubali toba
kutubu kipindi hiki ni kitu chema kabisa ambacho twaweza kufanya ili kuandaa
kuja kwa Kristo daima katika maisha yetu.
Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuziona dhambi zangu kadiri tunavyozama katika kipindi
hichi cha majilio. Nisaidie niweze kutambua yale yote yanayonifanya niwe mbali
nawe na kuyaacha kwa moyo wote. Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment