“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Desemba 3,
Juma
la 1 la majilio.
Isa.
29:17-24;
Zab
27:1,4,13-14;
Mt
9:27-31
KUTAMBUA
UPOFU WETU!
Karibuni
sana wapendwa wa Bwana kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana katika somo la injili, Bwana Yesu anawapatia vipofu uonaji. Hakika kukaa
katika upofu ni jambo gumu sana. Ni vigumu kujua ukweli wa mambo yanayoendelea.
Mengi tutaishiwa kudanganywa na wenzetu tu. Unapopata mwanga, ndipo unaweza
kuona kivyako na kuelewa maana halisi ya vitu.
Shetani
ndiye mwenye kutufanya vipofu. Mara nyingi hubovusha macho yetu, na kutufanya
tushindwe kuona faida iliyopo kwenye upande wa Mungu. Yeye atatuonesha na
kutufanya tuonje utamu uliopo katika ulevi, uasherati, na uvivu. Atatuzuia
tushindwe kuona utamu uliopo katika kusali, katika kuwasaidia wenzetu, na
kuwajali maskini. Sisi tuombe siku zote Mungu atupatie Mwanga. Atuondolee upofu
wetu. Atufanye tufungue macho yetu tupate kuona faida iliyopo katika kukubali
kukaripiwa, na kuishi hata na wale marafiki ambao tunadhania kwamba wanaingilia
sana maisha yetu lakini kwa upande mwingine wanatupatia faida kwani hutulinda
kwa maisha na mifano yao bora.
Katika
somo la kwanza, linatoa habari juu ya ujio wa siku; siku ya matumaini kwa
wanyenyekevu na walio katika giza. Siku hiyo inatangazwa kuwa nzuri kwa
Lebanoni, inatangazwa kuwa nzuri kwa vipofu, na viziwi. Mwenye kuonea wengine
ataangamizwa, na mwenye dharau atakoma kabisa. Wengi watapata kumfahamu
Mwenyezi Mungu.
Hakika
hii ni siku ya furaha, na Yesu mwenyewe ndiye atakayeikamilisha. Wanadamu huwa
hatudumu kwenye nguvu zetu, au cheo chetu au afya yetu hadi mwisho.
Sisi
ipo siku sisi tulio na majivuno tutakoma. Yesu ndiye mwenye kubaki milele.
Alipokuja kwa mara ya kwanza alituonjesha kile atakachokamilisha ajapo kwa mara
ya pili. Hivyo tujifunze kuwa na tabia za kinyenyekevu, tujue kwamba tunaisubiri
siku nzuri, siku ya furaha. Hata na wale tunaoumwa, hakika tujue kwamba siku ya
namna hiyo itakuja kwetu. Ipo siku Bwana ataondoa na kufuta machozi yote.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment