“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumma,
Desemba 31, 2021,
Oktava
ya Kuzaliwa Bwana
1
Yoh 2: 18-21;
Zab
96: 1-2, 11-13;
Yn
1: 1-18
KUITIKA
NAKUTOA JIBU KWA NENO LA MUNGU!
Ndugu zangu karibuni kwa adhimisho
la Misa Takatifu asubuni ya leo. Fumbo la umwilisho linaloelezewa na injili ya
leo la Neno aliye Mungu kutwaa ubinadamu lilileta ugumu katika kulielewa na
kuliamini. Baadhi hawakulipokea bali walitunga maelezo tofauti kulielezea na
hivyo palitokea manabii wa uongo. Baadhi yao walikuwa ni Wadoketi (Docetists)
waliosisitiza kwamba Yesu alifanania kama binadamu tu lakini kwa undani, hakuwa
binadamu. Wengine walikataa Umungu wa Yesu kabisa. Kuendana na 1 Yoh 4:1-3,
hawa kwa ujumla hawakuamini Yesu Kristo kuwa mwana wa Mungu na kwamba alikuja
kwa njia ya mwili. Ila kwa sababu Mtume Yohane aliishi kwa muda mrefu, ilimbidi
apinge uzushi wa manabii hawa kama anavyofanya katika somo la kwanza.
Nyakati zetu pia zimezidi kwa
manabii wa uongo. Wengine wanamuona Yesu kuwa kama ATM, wengine kama mtoa raha
tu, wengine hawamkubali kama Mungu. Huu ni mwaliko kwetu kwamba lazima tukatae
aina hizi za upotoshaji na kumhubiri Kristo sawasawa.
Yohane katika somo la kwanza
anaendelea kuzungumzia juu ya ujio wa manabii wa uongo. Anasema kwamba mwanzoni
walikuwa wakristo miongoni mwa jamii ya waamini lakini wakaamua kwenda kivyao.
Nabii wa uongo ni wa kuogopwa kwani hupotosha jamii yote ya waamini kirahisi
kwani ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo. Siku hizi wengi
wamekwishapotoshwa na manabii hawa.
Sisi basi habari hizi tumezisikia
lakini ni huzuni sana kwani manabii wa uongo wamekuwa wakiibuka kila siku na
wamekuwa wakipata wafuasi kila kukicha. Sisi tuombe kuwatambua manabii hawa wa
uongo na kuwapinga. Tuepuke pia kishawishi cha kujitenga na jamii ya waamini.
Hiki ni chanzo kikuu cha manabii wa uongo. Ndani ya kanisa tutashinda, nje ya
kanisa hatuwezi chochote.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment