“ASALI
ITOKAYO MWABANI”
Desemba
30, 2021.
------------------------------------------------
ALHAMISI,
OKTAVA YA NOELI
Somo
la 1: 1 Yn 2:12-17 Yohane anaendelea kutuhubiria sisi tena na kutukumbusha juu
ya jukumu letu kama Wakristo, na hasa juu ya sisi kuwa macho kwasababu ya
malimwengu.
Wimbo
wa Katikati Zab: Ps 95: 7-10 Mbingu na zifurahi nchi na ishangilie. Mwabuduni
Bwana hekaluni mwake. Ee Dunia tetemeka mbele za Bwana.
Injili:
Lk 2: 36-40 Anna, nabii mwanamke, anasali kwa ujasiri kama Simeoni kwa ajili ya
Mkombozi. Wakati alipo muona, na kumpa Mungu shukrani na anaondoka na kwenda
kumwambia kila mmoja kuhusu hili.
------------------------------------------------
JIBU
LA KUKUMBANA NA KIPINDI CHETU CHA NOELI
Ndugu zangu katika Kristo karibuni
kwa adhimisho la Misa takatifu, kikubwa tunachokutana nacho katika masomo yetu
ni kuhusu, Kukutana na Mtoto Yesu: Nabii Anna tunayemsikia katika Injili
hakufungwa na ya dunia. Yeye baada ya kifo cha mume wake aliyatolea maisha yake
yote kwa Mungu. Kupendelea kwake kukaa hekaluni kulimbahatisha kuwa miongoni
mwa watu wa kwanza kukutana na Masiha wa Israeli.
Hii iliwezekana kwa sababu hakuwa
mtumwa wa dunia kama somo la kwanza linavyotuambia. Nasi tuepuke kuyapenda ya
dunia. Tutafute ya mbingu. Tusipofungwa na tamaa za kidunia na kupania ya
mbingu hakika tutakutana na mtoto Yesu, Masiha wetu kama Nabii Ana alivyokutana
naye. Tuzoee kusoma maandiko matakatifu, kujitolea kwa ajili ya kanisa na
kuwasaidia makuhani na watawa. Tuepuke kukaa maeneo yawezayo kukwaza Imani zetu
au za wengine. Namna hii tutaweza kukutana na mtoto Yesu na kumshukuru Mungu
kama ilivyotokea kwa Nabii Anna.
Tumuombe Roho Mtakatifu tukisema,
Ee Roho Mtakatifu naomba unisadie niandae mazingira ambayo nitaweza kukutana na
mtoto Yesu daima.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment