“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu,
Desemba 13, 2021,
Juma
la 3 la Majilio
Hes
24: 2-7, 15-17;
Zab
24: 4-9;
Mt
21: 23-27
JE
UNAKUBALI NGUVU NA MAMLAKA YA YESU?
Injili
ya leo inaelezea juu ya mafarakano yanayo tokea kati ya Yesu na viongozi wa
dini wa wakati huo, baada ya kuwatoa wafanya biashara nje ya Hekalu (Mt
21:12-13). Mungu-Mwenyezi, katika nafsi ya Yesu Mwanae wa tangu milele yote,
alikuwa akifundisha maneno ya uzima. Aliongea kwa nguvu na mamlaka na kila mtu
alitambua hilo. Lakini Makuhani na Wakubwa wanaonekana wakipata hasira na wivu
juu yake , huku wakimuuliza amepata wapi mamlaka? Hili swali linaonesha ni kwa
jinsi ghani hawa viongozi wa dini walivyokuwa mbali na ukweli, walikuwa kipofu
kabisa. Hawakufungua moyo kupokea ukweli na wala hawakuwa tayari kufungua moyo
na kupokea ukombozi wa Mungu katika maisha yao. Na badala yake walisongwa na
ubinafsi, majivuno na wifu. Waliogopa kama watakubali kwamba Yohane Mbatizaji
na Yesu, utume wao umetoka Mbinguni, watapoteza umaarufu wao juu ya watu na
watapoteza mamlaka yao juu ya watu.
Sisi
wote tuna uongozi katika hali flani. Hata mazungumzo kati ya watu wawili, kila
mtu anamamlaka flani. Kama ulikuwa kwenye hilo hekalu wakati Yesu anaongea,
ungejibu nini au ungefanya nini? Je, ungemkataa? Je, ungetamani kumsikiliza
zaidi? Je, utakasirishwa nae au kuwa na wivu naye? Je, utatambua nguvu yake ya
Kimungu, upendo, mamlaka nakumtafuta yeye? Sisi pia wakati mwingine katika
maisha yetu, tunajidanganya na kukimbia ukweli, tunataka tutawale kila kitu
bila hata ya Kumruhusu Mungu afanye mabadiliko katika maisha yetu. Leo, tuamue
na kukubali kupokea nguvu ya Mungu na tumruhusu yeye awe dereva wa maisha yetu
katika furaha na ukamilifu wote.
Sala:
Bwana, nisaidie kuisikia sauti yako ya utakatifu kila mahali. Nisaidie niweze
kukutambua wewe kila mahali ninapoenda. Na ninapo kutafuta nisaidie nifurahi
kwa kukupata wewe na kukubali yote kwa ujasiri unayosema. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment