“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Desemba 15, 2021
Juma
la 3 la Majilio
Is
45: 6-8, 18-25;
Isa
45: 6-8, 18-25;
Zab
85: 8, 9-13;
Lk
7: 19-23.
JE,
NI YESU UNAMSUBIRIA?
Katika
Injili ya Luka leo, Yohane Mbatizaji anawaagiza Wafuasi wamuulize Yesu, “Je, ni
yeye ajaye au tumtazamie mwingine?” Hili pia ni swali la muhimu sana lililopo
ndani kabisa mwa moyo wa kila mmoja wetu, je ni ‘wewe’ ninayekusubiri, ‘ambaye’
nimekusubiri maisha yangu yote? Na Yesu anakuwa nashauku ya kumjibu Yohane na
sisi pia, Yesu anatoa jibu hili: “Nendeni mkamwambie Yohane mliyo yaona ninyi na
kusikia, vipofu wanapona, viwete wanatembea, wakoma wanaponywa, viziwi wanapata
kusikia na waliokufa wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema”. Kwa
maneno mengine, Yesu anatujibu sisi akisema,”mimi ndiye unayemsubiri, ambaye
amekuja kukuokoa na kufanya mambo yote mapya”
Injili
hii inatualika tuyaseme maswali yetu yaliyo ndani kabisa mwa mioyo yetu, na kwa
nguvu kabisa ya unyenyekevu kama wa Yohane, tumuulize Yesu kilichopo ndani
kabisa mwa mioyo yetu. Yesu anatamani kututimizia hamu ya mioyo yetu, atafanya
hivyo tuu kama sisi tutaonesha unyenyekevu wa kumwomba, kwasababu Yesu
haingilii uhuru wa mwanadamu. Ni jukumu letu tuchague lililo sahihi tutumie
uhuru wetu vizuri na kumwomba yeye, kwani kwa hakika yupo tayari kutimiza
tunayotaka kumwomba.
Tunaomba
kipindi hiki cha Majilio kiwe kipindi cha kumtambua Yesu, ukweli, ambao
tunautafuta. Tuzamishe mawazo yetu kwake tuweze kusikia yale yote anayotaka
kutuambia Bwana wetu.
Sala:
Bwana, nisaidie katika kipindi hiki cha majilio kuendelea kuandaa moyo wangu.
Nisaidie nisikie maneno yako na yote unayotaka kusema nami. Naomba nikufuate
katika yote na kati ya yote nikutambue wewe kama Mwokozi wa maisha yangu,
Mkombozi ambaye nimemsubiria katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment