“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 18, 2021.
Juma
la 33 la Mwaka
1
Mak 2: 15-29;
Zab
50: 1-2, 5-6, 14-15 (K) 23;
Lk
19: 41-44.
YESU
ANALIA JUU YA YERUSALEMU
Albert
Schweitzer ni mwanamuziki mkubwa kutoka Ujerumani, alikuwa mtoto wa mchungaji,
mpiga kinanda maarufu. Alikuwa na astashahada ya falsafa na elimu ya Mungu.
Akiwa na miaka 30, alisoma ujumbe mmoja wa Mmisionari mmoja kutoka katika
gazeti kuhusu hitaji kubwa la madktari Afrika. Akiwashangaza wengi kwa kwenda
Gabon, Magharibi ya kati mwa Afrika. Alitumia fedha zake kujenga eneo kwa ajili
ya wakoma. Dr. Albert Schweitzer aliandika : "siku moja katika kuchoka
kwangu nilijirusha katika kiti katika chumba ambacho kilikuwa cha kuongea na
watu, na huku akilalamika! Hivi nilikuwa na upungufu ghani kuja kuwa daktari
katika maeneo ya mateso kama haya? Daktari mmoja msaidizi akamjibu, ni kweli
Dr, hapa duniani kuna mateso lakini sio mbinguni”. Baadae Dr. Albert Schweitzer
aliandika “sijui mwisho wako utakuwa nini, mimi nina hakika na kitu kimoja:
kati yenu watakao kuwa wenye furaha kweli ni wale waliogundua kutoa faraja na
kutumikia”.
Katika
somo la kwanza tunamuona Mfalme Atioko akiwaamuru Wayahudi wote watolee sadaka
miungu ya Kigiriki. Matiasi hakukataa tu kufanya hivyo bali kufanya hivyo. “
aliwaua Wayahudi waliosogea na kutaka kufanya hivyo. Alisema “mimi na watoto
wangu na kaka na ndugu zangu tutaishi kadiri ya Agano la Baba zetu” (1Mak 2:
20). Katika Injili ya leo Yesu anaulilia mji wa Yerusalemu. Kilio cha Yesu ni
ishara ya unabii. Kama nabii Elisha alivyo lia juu ya Israeli, kwa kutabiri
mateso (2Falm 8:7-15), Yesu anafanya hivyo pia kabla ya kifo chake. Mji wa
Yerusalemu ulikuwa na bahati baada ya bahati ya ukombozi wao, Amani na ukuu,
lakini watu waliacha tu nakujilalia tu kama vile nafaka juu ya mchanga. Alivyo ukaribia
na kuuona vizuri mji, alitambua mara moja kwamba watu wengi watamkataa na
watakataa ujio wake. Alikuja kuwaletea zawadi ya uzima wa milele. Mbaya ni
kwamba wengi walimkataa Yesu kwasababu ya kumuona sio muhimu na wengine
walipata hasira juu yake na kupanga kifo chake. Yesu alikuwa haulilii tu mji wa
Yerusalemu. Analia kwasababu ya ukosefu wa Imani ambao watu wengi wanayo. Yesu
alitambua hili na lilimumiza sana na kumhuzunisha moyoni.
Tutafakari
leo juu ya kishawishi cha kuona Yesu sio muhimu na juu ya ujumbe wake. Ngoa
hali hii ya kuto kumuona Yesu ni muhimu ndani mwako na amua kupanga upya
kumtumikia na kushika mapenzi yake matakatifu kwa moyo wote. Kama Dr Albert,
ambaye kwa moyo wote aliamua kuacha mambo mengi huko Ulaya na kuamua kuja
kuwatumikia watu huku Afrika au Matiasi ambaye aliona ni bora kufa kuliko
kuacha kumtii Mungu. Je, upo tayari kumkaribisha Yesu ndani ya moyo wako au
unamkataa kama Yerusalemu walivyo mkataa?
Sala:
Bwana, ninaomba ungoe kitu chochote kisicho endana na mapenzi yako ndani ya
moyo wangu. Unapo lia kwasababu ya dhambi zangu, ninaomba machozi haya yanioshe
mimi na kunitakasa ili niweze kufanya wongofu wa kweli ukiwa kama Bwana wangu
na mfalme wangu. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment