MASOMO
YA MISA NOVEMBA 18, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
1Mak.
2:15-29
Watumishi
wa mfalme waliokuwa wakiwashurutisha watu kuasi wakaja Modini kuwalazimisha
hata Matathia na wanawe walikuwapo. Watumishi wa mfalme wakamwambia Matathia,
Wewe u kiongozi, mtu mkuu, maarufu katika mji huu. Una wana wako na ndugu zako
wa kujiweka upande wako. Basi, tangulia wewe, uitimize amri ya mfalme, kama
walivyofanya watu wote wa mataifa, na watu wa Uyahudi, nao waliosalia
Yerusalemu. Ndipo wewe na wana wako watahesabiwa kati ya rafiki za mfalme;
naam, wewe na wana wako watatuzwa fedha na dhahabu na vipawa vingi.
Matathia
akajibu, akasema kwa sauti kuu, Hata mataifa yote katika milki ya mfalme
wakimtii, wakiacha kila mtu dini ya wazee wake na kuchagua kuzifuata amri za
mfalme, lakini mimi sivyo. Mimi na wanangu na ndugu zangu tutaishika njia ya
agano la baba zetu. Isiwe kwetu kujitenga na sheria na maagano, hasha! Sisi
hatutaisikiliza amri ya mfalme tugeuke katika dini yetu, kwa kuume wala kwa
kushoto.
Alipokwisha
kusema hayo, Myahudi mmoja alijitokeza machoni pa watu wote kusudi atoe dhabihu
juu ya madhabahu iliyokuwapo Modini, kama ilivyoamriwa na mfalme. Matathia
alipomwona, alishikwa na uharara, moyo wake ukatetemeka. Hasira yake ikatokeza
hukumu, akamwendea mbio, akamwua pale madhabahuni. Kisha alimwua yule mtu wa
mfalme naye, aliyekuwa akiishurutisha dhabihu, akaiangusha madhabahu. Hivyo
alionyesha juhudi yake kwa sheria, kama juhudi ya Finehasi juu ya Zimri, mwana
wa Salu.
Kisha,
Matathia alipiga mbiu mjini kwa sauti kuu, akisema, Kila aliye na juhusi kwa
ajili ya sheria na kutaka kulitetea agano, na anifuate! Naye na wana wake
wakakimbilia milimani, wakiviacha vyote walivyokuwa navyo mjini.
Ndipo
wengi waliokuwa wakitafuta haki na hukumu walikwenda jangwani wafanye maskani
yao huko.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
50:1-2,5-6,14-15 (K) 23
(K)
Nitawaonyesha wokovu wa Mungu.
Mungu,
Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka
maawio ya jua hata machweo yake.
Tokea
Sayuni, ukamilifu wa uzuri,
Mungu
amemulika. (K)
Nikusanyieni
wacha Mungu wangu,
Waliofanya
agano nami kwwa dhabihu.
Na
mbingu zitatangaza haki yake,
Kwa
maana Mungu ndiye aliye hakimu (K)
Mtolee
Mungu dhabihu za kushukuru,
Mtimizie
Aliye juu nadhiri zako.
Ukaniite
siku ya mateso;
Nitakuokoa,
na wewe utanitukuza. (K)
SHANGILIO
Yn.
14:5
Aleluya,
aleluya,
Bwana
anasema: Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima, mtu haji kwa Baba, ila kwa njia
ya mimi.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:41-44
Yesu
alipofika karibu ya Yerusalemu aliuona mji, akaulilia, akisema, Laiti
ungalijua, hata wewe, katika siku hii, yapasayo Amani! Lakini sasa yamefichwa
machoni pako. Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma,
likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe
na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua
majira ya kujiliwa kwako.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment