“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Novemba 4, 2021,
Juma
la 31 la mwaka wa Kanisa
Warumi
14:7-12
Zaburi
27:1,4,13-14 (K)13
Luka
15:1-10
Ndugu
zangu wapendwa, karibuni kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana leo, Mtume Paulo anawaeleza Warumi kwamba wao wanajulikana machoni pa
Bwana. Maisha yao yote yapo katika mkono wa Bwana. Hata kama watakufa au kama
wataishi, hakika bado wanazidi kubakia wa thamani machoni pa Bwana. Na kwa
hakika hakuna hata unywele wa vichwa vyao utakaopotea au kusahaulika pale
wawapo na Bwana.
Kristo
anamiliki wote, waliokufa na wanaoishi. Hivyo hakuna haja ya kudharauliana au
kuwahukumu wenzetu na kuwaona kama wasiofaa-wote ni wakristo. Hata kama ni
wagonjwa kiasi kwamba hawawezi chochote, hata kama wana njaa ya ajabu, hata
kama wanashindwa kupata mlo wa mchana, hata kama ni wadhambi kiasi gani-wote ni
mali ya Mungu. Ni Mungu aliyewaumba ni mali yake.
Paulo
anatoa ujumbe huu kwa Wakristo wa Roma kwa sababu kipindi walioongokea ukristo
walikuwa watu wa aina mbalimbali. Baadhi walikuwa watumwa, wengine wagonjwa,
wengine maskini-hivyo kulikuwa na urahisi wa kuanza kudharauliana na
kuhukumiana. Pia kulikuwa na kishawishi cha wao kushindwa kukaa pamoja ndani ya
kanisa. Yeye anawaeleza kwamba jueni kwamba wote ni mali ya Kristo. Hata kama
nyumbani mwake hawezi kula nyama, anakula tu matembele bado anazidi kubakia
mali ya Kristo.
Sisi
tujifunze kuwapenda wote, tujue kwamba wenzetu hata kama wapoje wanazidi
kubakia mali ya Kristo. Na hakika nao pia watauona wema wa Mungu kwani ni wana
wake. Tujifunze kuwaheshimu wenzetu wote. Tuone aibu pale matabaka yanapoanza
kuingia ndani ya kanisa, na watu kukoseana upendo na kuchukiana. Wenzetu wote
ni mali ya Kristo. Tuwapende.
Katika
injili, Bwana Yesu anazidi kutuonesha jinsi kila mwanadamu alivyo wa thamani
machoni pa Mungu. Mungu yupo tayari kutumia gharama kubwa ili kumfanya
asipotee. Tayari alikwishatumia gharama kubwa kwa kumtoa mwanae wa pekee ili
amkomboe mwanadamu mtumwa.
Hivyo
nasi tufuate mfano wa Mungu tuwaone wenzetu kuwa bado wanazidi kubakia wa
thamani kubwa machoni pa Mungu. Tuwe watu wa kujitoa zaidi kwa ajili ya
maendeleo ya wenzetu. Wenzetu wengi wanaumia kwa sababu bado hatujajitolea
zaidi kwa ajili yao. Sisi tunatabia ya kujenga matabaka. Tunawapendelea watu
wenye vyeo na sura fulani fulani. Wapo tunaopendelea wanadamu weupe, warefu na
kuwachukia weusi na wafupi. Wapo tunaowastahi wenye fedha na kuwadharau walio
maskini. Hatupaswi kuonesha hili. Tuwaheshimu wote. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment