“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano
, Desemba 1, 2021
Juma
la 1 la majilio
Isa.
26:1-6;
Zab
118:1,8-9,19-21,25-27;
Mt
7:21.24-27
NI
KITU GHANI KINATUFANYA TUSITIKISIKE?
Karibuni
sana ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno
la Bwana katika Zaburi yetu ya wimbo wa katikati inazungumzia juu ya furaha na
tamaa ya kutaka kukaa katika nyumba ya Bwana. Hakika kukaa kwenye nyua za
Bwana, kuna faida zaidi kwani kukaa tu karibu yake litatuwezesha kukwepa
madhambi mengi. Mara nyingi mazingira mabaya hutusababishia vishawishi, na
wengi wetu tunaanguka dhambini baada ya kujiweka kwenye mazingira mabaya. Yafaa
tupendelee kukaa kwenye mazingira yaliyo karibu na Bwana. Na kwa hakika
tutashinda mengi.
Kipindi
cha Majilio na kipindi cha kukaa karibu na Bwana.
Katika
somo la injili, Makutano wamejitahidi kukaa na Bwana kwa muda mrefu. Na kwa
kuwa wamekaa na Bwana, Bwana hawaachi waondoke pweke bali anawapatia chakula
pia. Yesu hakutaka wakafie njiani, aliwapatia chakula bila ya wao kutegemea.
Ndivyo ilivyo, ukikaa karibu na Bwana, Bwana atatujali.
Leo
amewapatia makutano chakula. Hakika na sisi tusichoke kusali na kujiweka karibu
na Bwana zaidi na zaidi.
Kwenye
somo la kwanza, Nabii Isaya anatangaza ujumbe wa matumaini kwamba upo wakati
ambapo aibu yetu na machozi yetu yatafutwa. Na Bwana atatuandalia karamu kuu
kabisa, yenye utamu wa ajabu. Hakika kila mmoja wetu anaitamani siku hii.
Macho
yetu na nyuso za wengi wetu zimejaa aibu. Tuna aibu ya magonjwa mbalimbali,
tuna aibu ya umaskini na njaa na yote haya yanafanya nyuso zetu zijae aibu. Kwa
hakika tunamhitaji Yesu afute aibu yetu. magonjwa yametupiga baadhi yetu hata
tunakosa sura. Njaa imetudhoofisha baadhi yetu. Hakika tumejaa aibu sana kwa
umaskini. Tumtegemee Yesu. Kwa hakika atafuta machozi yetu.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment