MASOMO
YA MISA DESEMBA 1, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 1 LA MAJILIO
SOMO
1
Isa.
25:6-10
Siku
ile Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya
divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta,
karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. Naye katika
mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule
uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana Mungu
atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika
ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo.
Katika
siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja
atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu
wake.
Kwa
maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
23:1-3,5-6 (K) 6
(K)
Nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Bwana
ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa
na kitu.
Katika
malisho ya majani mabichi hunilaza. (K)
Kando
ya maji ya utulivu huniongoza,
Hunihuisha
nafsi yangu na kuniongoza.
Katika
njia za haki kwa ajili ya jina lake. (K)
Waandaa
meza mbele yangu,
Machoni
pa watesi wangu.
Umenipaka
mafuta kichwani pangu,
Na
kikombe changu kinafurika. (K)
Hakika
wema na fadhili zitanifuata,
Siku
zote za maisha yangu;
Nami
nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Tazama
Bwana atakuja kuwaokoa watu wake, Heri walio tayari kumlaki.
Aleluya.
INJILI
Mt.
15:29-37
Siku
ile: Yesu alifika kando ya bahari ya Galilaya; akapanda mlimani, akaketi huko.
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na
wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya; hata ule mkutano
wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete
wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.
Yesu
akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia mkutano, kwa kuwa yapata siku
tatu wamekaa pamoja nami, wala hawana kitu cha kula; tena kuwaaga wakifunga
sipendi, wasije wakazimia njiani. Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi
mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii? Yesu
akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba, na visamaki vichache.
Akawaagiza
mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru
akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote
wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, makanda saba, yamejaa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment