Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, NOVEMBER 29, 2021

 

MASOMO YA MISA, NOVEMBER 29, 2021

JUMATATU, JUMA LA 1 LA MAJILIO

SOMO

Isa 4:2-6

Siku hiyo, chipukizi la Bwana litakuwa zuri, lenye utukufu na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka. Tena itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa mtakatifu; yaani. kila mmoja aliyeandikwa miongoni mwa hao walio hai ndani ya Yerusalemu.

Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake. kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza. Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni. na juu ya makusanyiko yake. Bwana ata umba wingu na moshi wakati wa mchana na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara. Kisha kutakuwa na hema kuwa uvuli wakati wa mchana kwa sababu ya hari, na kuwa mahali pa kukimbilia na kujificha wakati wa tufani na mvua.

Neno la Bwana…….Tumshukuru Mungu..

WIMBO WA KATI KATI Zab. 122 : 1-4. 8,9 (K) 1

1. Nalifurahi waliponiarabia,

Na twende nyumbani kwa Bwana.

Miguu yetu imesimama

Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

(K) Nalifurahi waliponiambia,

Na twende nyumbani kwa Bwana.

Ee Yerusalemu ulivejengwa Kama mji ulioshikamana,

Huko ndiko walikopanda kabila Kabila za Bwana. (K)

Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa. Amani ikae nawe

Kwa ajili ya nyumba ya Bwana. Mungu wetu Nikutafutie mema. (K)

SHANG1LIO

Zab. 80 :4

Aleluya, aleluva.

Ee Bwana, Mungu wa majeshi, hata lini?

Utayagadhabikia maombi ya watu wako?

Aleluya.

INJILI

Mt. 8:1-11

Yesu alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye. Yule akida akamjibu, akasema, Bwana. mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno moja tu, na mtumishi wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu. Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanva. Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa yeyote katika Israeli. Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu na Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni.

Neno la Bwana…………Sifa kwako Ee Kristo.

 

Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

 

No comments:

Post a Comment