MASOMO
YA MISA NOVEMBA 8, 2021
JUMATATU
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Hek.
1:1-7
Pendeni
haki, enyi waamuzi wa dunia; Tafakarini habari za Bwana kwa moyo mwema. Na
kumtafuta katika unyofu wa moyo. Kwa sababu huonekana nao wasiomjaribu, na kufunuliwa
kwao wasiokosa kumwamini. Mradi fikira zilizopotoka hutenga wanadamu na Mungu,
na enzi yake ikijaribiwa, huwafadhaisha wajinga.
Hekima
haiingii katika roho ya mtu awazaye maovu, wala haikai katika mwili wa mtu
aliyefungwa rehani na dhambi. Kwa kuwa roho takatifu yenye maadili huikimbia
hila, hubumburuka kujiepusha na fikira zisizo na akili, hufadhaika kuingiwa na
udhalimu.
Maana
Hekima ni roho ambayo huwapenda wanadamu, wala haimwachilii mkufuru hatia ya
midomo yake; kwa sababu Mungu huvishuhudia viuno vyake, na kuusimamia hasa moyo
wake, na kuusikiliza ulimi wake. Roho ya Bwana imeujaza ulimwengu, nayo
inayoviungamanisha viumbe vyote hujua maana ya kila sauti.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
139:1-10
(K)
Uniongoze katika njia ya milele, Ee Bwana.
Ee
Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe
wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu
wazo langu tokea mbali.
Umepepeta
kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa
na njia zangu zote. (K)
Maana
hamna neno ulimini mwangu
Usilolijua
kabisa, Bwana.
Umenizingira
nyuma na mbele,
Ukaniwekea
mkono wako.
Maarifa
hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi,
Hayadirikiki,
siwezi kuyafikia. (K)
Niende
wapi nijiepushe na roho yako?
Niende
wapi niukimbie uso wako?
Kama
ningepanda mbinguni, Wewe uko,
Ningefanya
kuzimu kitanda changu, Wewe uko. (K)
Ningezitwaa
mbawa za asubuhi,
Na
kukaa pande za mwisho za bahari;
Huko
nako mkono wako utaniongoza,
Na
mkono wako wa kuume utanishika. (K)
SHANGILIO
2Kor.
5:19
Aleluya,
aleluya,
Mungu
alikuwa ndani ya Kristu, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani
yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
INJILI
Lk.
17:1 – 6
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule
ambaye yaja kwa sababu yake! Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusaga lifungwe
shingoni mwake, akatupwe baharini, kulikko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
Jilindeni.
Kama
ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika
siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Mitume
wakamwambia Bwana, Tuongezee Imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na Imani kiasi
cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka ukapandwe baharini, nao
ungewatii.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment