“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Novemba 8, 2021.
Juma
la 32 la Mwaka
Hek
1:1-7;
Zab
138:1-10;
Lk
17:1-6
KUWA
CHANYA KATIKA ULIMWENGU HASI
Karibuni
sana wapendwa wa Bwana kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana katika somo la kwanza tunasikia kuhusu habari za hekima. Ni tunu ambayo
kila mmoja anapaswa kuitamani, ni tunu itokayo kwa Bwana, hekima ni Takatifu.
Hekima huja pale tunapojizatiti na kuanza kupendelea mema, kutenda haki. Waweza
kuwa na elimu kubwa sana, au na vipaji vizuri sana lakini kama hupendelei haki
na mema hakika huwezi kuwa na hekima. Hivyo tujifunze kupenda mema.
Mara
nyingi kuchagua kutenda dhambi kunachaguliwa kwa kirahisi zaidi kuliko kutenda
mema. Dhambi inachaguliwa zaidi kuliko mema. Siku zote kitu rahisi kina gharama
kubwa. Hivyo duniani ni wachache tu wenye hekima. Hivyo tujitahidi kuendelea
kupenda kutenda mema. Vipaji vyetu, kazi na vyeo vyetu vimeshindwa kuisaidia
jamii kwa sababu ya kupendelea kuvutiwa na urahisi wa kutenda dhambi kuliko
mema. Tupendelee yaliyo mema.
Hivyo
tuangalie kazi tunazofanya, lazima nihakikishe kwamba kazi zetu tunazitenda kwa
wema na haki. Kama ni wafanya biashara, tusiwauzie watu bidhaa mbovu au fake.
Tupendeleee kuwafanyia watu vitu vizuri.
Katika
somo la injili, Bwana Yesu anaelezea juu ya adhabu itakayotolewa kwa yeyote
mwenye kumkwaza aliye mdogo. Adhabu yake ni kufungiwa jiwe shingoni na kutupwa
baharini. Adhabu hii inafanana na ile aliyopewa joka pale alipokuwa muasi
mbinguni. Alitupwa chini na kao lake kuondolewa (Uf 12) na hivyo hakuna hata
alama yake iliyosalia.
Adhabu
ya mtu anayekwaza wadogo nayo ni kufungiwa jiwe ili naye apotee ili asije
akaacha kitu cha kuendelea kukwaza watu waache kumfuata Kristo.
Hivyo
tuogope dhambi ya kukwaza wenzetu. tukiendelea kukwaza adhabu yake ni kali,
yenye kufanana na ile aliyopewa mkuu wa uovu wote, lile joka kubwa (Uf 12).
Tuwe mfano mzuri kwa wadogo zetu. tuwaoneshe mfano mzuri. Tuongee nao maneno
mazuri, tuepuke kutumia lugha mbaya kati yao, tusiwafundishe ukatili, matusi au
uchafu wote. Kila mmoja ampende aliye mdogo.
Pia
Yesu anasisitiza juu ya kusamehe kwamba tusichoke kuwasamehe wenzetu. Wapo
wenzetu watakosea mara mia, na watakuja kila wakati kuomba msamaha lakini
tusichoke na yule anayetukosea na kuja kila siku kuomba msamaha. Wanadamu wengi
ni dhaifu hivyo tusisite kwenda kuomba msamaha kila tunapowakosea wenzetu na
sisi tusichoke kutoa msamaha kwa wenzetu. Kristo hutoa msamaha kwetu kila siku.
Nasi tusiache kutoa msamaha kwa wenzetu.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment