MASOMO
YA MISA NOVEMBA 30, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 1 LA MWAKA
SIKUKUU
YA MT. ANDREA, MTUME
SOMO
1
Rum.
10:9-18
Ukimkiri
Yesu kw akinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haki, na kwa kinyw ahukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye
hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule
ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila
atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
Basi
wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena
wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri
kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Lakini si wote walioitii ile
habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeazimia habari zetu?
Basi Imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini
nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote,
na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:1-4 (K)
(K)
Sauti yao imeenea duniani mwote.
Mbingu
zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na
anga laitangaza kazi ya mikono yake.
Mchana
husemezana na mchana,
Usiku
hutolea usiku maarifa. (K)
Hakuna
lugha wala maneno,
Sauti
yao haisikilikani.
Sauti
yao imeenea duniani mwote,
Na
maneno yao hata miisho ya ulimwengu. (K)
SHANGILIO
Mt.
4:18
Aleluya,
aleluya,
Bwana
asema, Nifuateni, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
Aleluya.
INJILI
Mt.
4:18-22
Yesu
alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni
aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa
wavuvi. Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. Mara
wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
Akaendelea
mbele, akanona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohane nduguye,
ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu
zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment