MASOMO
YA MISA NOVEMBA 3, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 31 LA MWAKA
SOMO
1
Rum.
13:8-10
Msiwiwe
na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza
sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani, na ikiwapo amri
nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako
kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu
wa sheria.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
112:1-2,4-5,9 (K)
(K)
Heri atendaye fadhili na kukopesha.
Aleluya,
Heri
mtu yule amchaye Bwana,
Apendezwaye
sana na maagizo yake.
Wazao
wake watakuwa hodari duniani;
Kizazi
cha wenye adili kitabarikiwa. (K)
Nuru
huwazukia wenye adili gizani;
Ana
fadhili na huruma na haki.
Heri
atendaye fadhili na kukopesha;
Atengenezaye
mambo yake kwa haki. (K)
Amekirimu,
na kuwapa maskini,
Haki
yake yakaa milele,
Pembe
yake itatukuzwa kwa utukufu. (K)
SHANGILIO
Mt.
11:25
Aleluya,
aleluya,
Nakushukuru,
Baba, Bwana wa mbingu nan chi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na
akili, ukawafunulia watoto wachanga.
Aleluya.
INJILI
Lk.
14:25-33
Makutano
mengi walipokuwa wakifuatana na Yesu, aligeuka, akawaambia, Kama mtu akija
kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu
zake waume kwa wake, na wanawe, na ndugu zake waume kwa wake; naam, na hata
nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu yeyote asiyeuchukua
msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Maana
ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu
gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya
kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu
alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. Au kuna mfalme gani, akitaka
kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba
yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na
watu elfu ishirini? Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za
Amani, mtu yule akali mbali. Basi, kadhlika kila mmoja wenu asiyeacha vyote
alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment