MASOMO
YA MISA NOVEMBA 26, 2021
IJUMAA
, JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Dan.
7:2-14
Danieli
alinena akisema, Naliona katika maneno yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo
pepo nane za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo wanyama wakubwa
wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama
simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka
manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama
mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. Na tazama, mnyama mwingine, wa
pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu
ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka,
ule nyama tena.
Kisha
nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine kama chui, naye juu ya mgongo wake
alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vine;
akapewa mamlaka. Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama
wanne, mwenye kutisha, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye
alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipange vipande, na
kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa
kwanza, naye alikuwa na pembe nne.
Nikaziangalia
sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa
ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa;
na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na mbacho kama macho ya mwanadamu, na
kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Nikatazama
hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake
yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti
chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama
wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara
elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
Nikatazama
wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe;
nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa
ateketezwe kwa moto. Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang’anywa
mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. Nikaona
katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja
na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Naye
akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote,
na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo haitapita
kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Dan.
3:75-81 (K) 59
(K)
Msifuni na kumwadhimisha milele.
Milima
na vilima, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Mimea
yote ya nchi, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Chemchemi,
mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Bahari
na mito, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Nyangumi
na vyote viendavyo majini,
Mhimidini
Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Ndege
zote za angani, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Hayawani
na wanyama wafugwao, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:29-33
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake mfano, Utazameni mtini na miti mingine yote. Wakati
iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno
yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo yamekwisha kuwa karibu. Nanyi
kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa
Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote
yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment