MASOMO
YA MISA NOVEMBA 24, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 34 LA MWAKA
SOMO
1
Dan.
5:1-6,13-14.16-17,23-28
Belshaza,
mfalme, aliwafanyia wakuu wake elfu karama kubwa, akanywa divai mbele ya elfu
hao. Belshaza, alipokuwa akionja ile divai, akaamuru wavilete vile vyombo vya
dhahabu na fedha, ambavyo baba yake, Nebukadreza, alivitoa katika hekalu
lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na
Masuria wake, wapate kuvinywea. Basi wakavileta vile vyombo vya dhahabu,
vilivyotolewa katika hekalu la nyumba ya Mungu lililokuwapo Yerusalemu; na
mfalme, na wakuu wake, na wake zake, na Masuria wake, wakavinywea. Wakanya
divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na
ya mti, na ya mwe. Saa iyo hiyo vikatokea vidole vya mkono wa mwanadamu,
vikaandika katika chokaa ya ukuta wa nymba ya enzi ya mfalme, mahali palipokikabili
kinara; naye mfalme akakiona kitanga cha ule mkono ulioandika. Ndipo uso wa
mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake
vikalegea; magoti yake yakagongana.
Ndipo
Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Na mfalme akanena, akamwambia Danieli, Je!
Wewe ndiwe DAnieli yule, aliye mmoja wa wana wa Yuda waliohamishwa, ambao
mfalme, baba yangu, aliwaleta huku toka Yerusalemu? Nimesikia habari zako,
kwamba roho ya miungu imo ndani yako, na kwamba nuru na ufahamu na akili bora
zimeonekana kwako. Nimesikia habari zako, kwamba waweza kuleta tafsiri, na
kufumbua mafumbo; haya! Kama ukiweza kulisoma andiko hili, na kunijulisha
tafsiri yake, utavikwa mavazi ya rangi ya zambarau, na kuwa na mkufu wa dhahabu
shingoni mwako, nawe utakuwa mtu wa tatu katika ufalme.
Ndipo
Danieli akajibu, akasema, mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe;
na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na
kumjulisha tafsiri yake. Basi umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta
vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na
Masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha nay a dhahabu, na ya
shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua
neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako I mkononi mwake, na njia zote ni
zake, hukumtukuza. Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele
zake, na maandiko haya yameandikwa.
Na
maandiko yaliyoandikwa ni haya; Mene, Mene, Tekeli, na Peresi. Na tafsiri ya
maneno haya ni hii; Mene, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. Tekeli,
umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. Peresi, ufalme wako
umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Dan.
3:62-67 (K) 59
(K)
Msifuni na kumwadhimisha Bwana milele.
Jua
na mwezi, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Nyota
za mbinguni, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Manyunyu
yote na ukungu, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Pepo
zote, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
Moto
na hari, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele.
Kipupwe
na musimu, mhimidini Bwana;
Msifuni
na kumwadhimisha milele. (K)
SHANGILIO
1Pet.
1:25
Aleluya,
aleluya,
Neno
la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa
kwenu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:12-19
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake; Watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya
masinagogi, na kuwatia magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa
ajili ya jina langu. Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu. Basi, kusudieni mioyoni
mwenu, kutofikirifikiri kwanza mtakavyojibu; Kwa sababu mimi nitawapa kinywa na
hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga. Nanyi
mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao
watawafisha baadhi yenu. Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.
Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Nanyi kwa subira yenu
mtaziponya nafsi zenu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment