MASOMO
YA MISA NOVEMBA 20 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
1Mak.
6:1:13
Mfalme
Antioko alipokuwa akisafiri katika nchi za juu alisikia habari za Elimaisi, mji
wa Uajemi, uliosifiwa sana kwa utajiri wake, fedha yake na dhahabu yake. Hekalu
lake lilikuwa na mali nyingi, na humo mlikuwa na ngao za dhahabu, na dirii, na
silaha za vita ambazo ziliwekwa humo na Iskanda, mwana wa Filipo, mfalme wa
Makedonia aliyekuwa wa kwanza kuwatawala Wayunani.
Basi,
alifika huko, akitaka kuutwaa mji na kuuteka nyara. Lakini haikuwezekana, kwa
sababu shauri lake lilijulikana kwa watu wa mjini, wakajipanga kufanya vita
naye. Akakimbia, akaondoka kwa moyo mzito kurudi Babeli. Akaletewa habari huko
Uajemi ya kuwa majeshi waliokwenda kuipiga nchi ya Uyahudi wameshindwa; tena
Lisia, aliyekwenda kwao na jeshi la nguvu sana, alikimbizwa mbele yao; nao
wamepata nguvu nyingi kwa sababu ya silaha na zana za vita na nyara
walizoziteka kwa majeshi waliyoyashinda. Zaidi ya hayo, wamelibomoa lile
chukizo alilolijengesha juu ya madhabahu Yerusalemu, na kupazungusha patakatifu
kuta ndefu, kama zamani, na mji wake Bethsura pia.
Ikawa,
mfalme alipoyasikia maneno hayo, alishikwa na bumbuazi akafadhaika mno. Akakaa
huko siku nyingi, maana alilemewa na huzuni nyingi hata alidhani atakufa.
Akawaita rafiki zake wote, akawaambia, Usingizi umefarakana na macho yangu,
hata moyo wangu umevunjika kwa taabu. Nasema ndani yangu, Jinsi nilivyosibiwa!
Ninazama katika maji mengi! Katika enzi yangu nalikuwa mstahiki, mwenye
kupendwa. Lakini sasa nayakumbuka mabaya niliyoyafanya Yerusalemu, jinsi
nilivyovichukua vyombo vyote vya fedha na dhahabu vilivyokuwapo, na kupeleka
majeshi kuwaharibu wenyeji wa Yerusalemu bila sababu. Nafahamu ya kuwa kwa
sababu hiyo maovu haya yamenipata, hata, tazama, ninakufa kihoro katika nchi ya
kigeni.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
9:1-2,5,15,18 (K) 15
(K)
Nitaufurahia wokovu wako, Ee Bwana.
Nitamshukuru
Bwana kwa moyo wangu wote;
Nitayasimulia
matendo yako yote ya ajabu;
Nitafurahi
na kukushangilia Wewe;
Nitaliimbia
jina lako, Wewe Uliye juu. (K)
Kwa
sababu adui zangu hurudi nyuma;
Hujikwaa
na kuangamia mbele zako.
Umewakembea
mataifa;
Na
kumwangamiza mdhalimu;
Umelifuta
jina lao milele na milele. (K)
Mataifa
wamezama katika shimo walilolifanya;
Kwa
wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
Kwa
maana mhitaji hatasahauliwa daima;
Matumaini
ya wanyonge hayatapotea milele. (K)
SHANGILIO
Efe.
1:17,18
Aleluya,
aleluya,
Mungu
wa Bwana wetu Yesu Kristu, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
20:27-40
Baadhi
ya masadukayo, wale wasemao ya kwamba hakuna ufufuo, walimwendea Yesu,
wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na dnugu
yake mwenye mke, lakini hana mtoto, na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake
mzao. Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; na
wa pili akamtwaa yule mke, akafa hana mtoto; hata wa tatu akamwoa, na kadhalika
wote saba, wakafa, wasiache watoto. Mwisho akafa yule mke naye. Basi, katika
ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba.
Yesu
akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao
kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi
wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika,
nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. Lakini, ya kuwa wafu
hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja
Bwana kuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Naye si
Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake. Waandishi wengine
wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema; wala hawakuthubutu kumwuliza neno
baada ya hayo.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment