MASOMO
YA MISA NOVEMBA 19, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 33 LA MWAKA
SOMO
1
1
Mak. 4:36-37,52-59
Yuda
na ndugu zake walisema, Sasa adui zetu wamevunjwa nguvu, basi tupande
tukapatakase mahali patakatifu na kupatabaruku. Jeshi lote likakusanyika
likapanda juu ya mlima Sayuni.
Wakaondoka
mapema siku ya ishirini na tano ya mwezi wa tisa, yaani Kislevu, mwaka mia
arobaini na nane, wakatoa dhabihu, kama ilivyoamriwa katika sheria, juu ya
madhabahu mpya ya sadaka za kuteketezwa waliyokuwa wameifanya. Wakati ule ule
na siku ile ile iliyotiwa unajisi na mataifa, siku ile ile iliwekwa wakfu tena
kwa nyimbo na vinubi na vinanda na matari. Watu wote wakaanguka kifudifudi
wakipaza sifa kwa mbingu, kwake aliyewapa ufanisi. Wakaiadhimisha sikukuu ya
kuitabaruku madhabahu muda wa siku nane, wakileta sadaka za kuteketezwa kwa
furaha na kutoa dhabihu ya wokovu na shukrani. Pia, waliupanda ukuta wa mbele
wa hekalu kwa taji za dhahabu na vigao; wakaweka wakfu malango na vyumba vya
makuhani na kuvitia milango. Kulikuwa na furaha kubwa kwa watu, na aibu
iliyoletwa na mataifa iliondolewa.
Yuda
na ndugu zake, na jamii yote ya Israeli, walikata shauri ya kuwa siku za
kuitabaruku madhabahu ziadhimishwe kwa furaha na shangwe kila mwaka kwa wakati
wake, muda wa siku nane tangu ishirini na tano ya mwezi Kislevu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Nya.
29:10-12 (K) 13
(K)
Tulisifu jina lako tukufu, Ee Bwana.
Uhimidiwe,
Ee Bwana,
Mungu
wa Israeli baba yetu,
Milele
na milele. (K)
Ee
Bwana, ukuu ni wako,
Na
uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi.
Utajiri
na heshima hutoka kwako. (K)
Wewe
watawala juu ya vyote,
Na
mkononi mwako mna uweza na nguvu,
Tena
mkononi mwako mna kuwatukuza,
Na
kuwawezesha wote. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Bwana
anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote
niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
19:45-48
Yesu
aliingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,
akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi
mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
Naye
akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi,
na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza; wasione la kutenda,
kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment