“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Novemba 19, 2021,
Juma
la 33 la Mwaka
1
Mac 4:36-37, 52-59
1
Ny 29: 10-12 (K) 13
Lk:
19:45-48
KUTAKASA
HEKALU LA MUNGU
Katika somo la kwanza tunamuona Yuda akipanda pamoja na Askari kwenda mlima Sioni ili kusafisha hekalu. Waandishi wa Kikrito hufananisha hekalu lisilo heshimiwa na roho iliyo jaa dhambi, na hekalu lilosafishwa na moyo uliomrudia Mungu. Hekalu lilikuwa na sehemu nne, kwanza eneo muhimu la kuabudu la makuhani, sehemu ya wanaume, sehemu ya wanawake na sehemu ya watu wa mataifa. Hivyo eneo hili lilibadilishwa na kuwa sehemu ya soko.
Wakati
wakuu wa hekalu hawajaingia ndani Yesu aliingia, Yesu aliingia na kuwafukuza
wote, kitendo hiki kilikuwa ni ishara kwa watu kwamba Mungu anatuchukulia sala
kwa makini sana. Yesu alishikwa na hasira na alisema kwamba “nyumba ya Baba
yangu ni nyumba ya sala sio pango la wanyanganyi”. Yesu yupo tayari kungoa uovu
wote kutoka katika hekalu la ulimwengu wetu, na yupo tayari kungoa uovu wote
kutoka katika hekalu la mioyo yetu.
Kila
roho ni hekalu ambalo linapaswa kuwekwa tayari kwa ajili ya utukufu wa Mungu na
kutimiza mapenzi yake matakatifu. Kwahiyo Injili hii itatimia kwetu kama
tutamruhusu Yesu aingie ndani ya mioyo yetu na kusafisha na kutufanya weupe.
Hili linaweza lisiwe jambo rahisi kwani linahitaji unyenyekevu wa kweli na
kujikabidhi kwake kweli lakini mwisho wake utakuwa ni kutakaswa na kuwa safi
kwa ajili ya Bwana wetu. Wakati Roho Mtakatifu alivyokuja kwetu kwa njia ya
utabatizo alisafisha dhambi zote na kutufanya hekalu la Mungu. Kwa msaada wake
tunapaswa tuhakikishe hekalu hili halichafuliwi. Kwani tunatambua kuwa kila
tunapotenda dhambi tuna muumiza Mungu.
Tafakari
leo kwamba Yesu anataka kutuletea utakaso katika njia zetu. Anatamani
kulisafisha kanisa pia, kila jamii na jumuiya, familia yako na roho yako
mwenyewe. Usikubali utakaso wa Yesu wenye nguvu takatifu ukupite. Sali kwa
utakaso wa kila namna na kwa kila ngazi na mwache Yesu atimize utume wake..
Sala:
Bwana, ninasali kwa ajili ya utakaso wa ulimwengu wetu, kanisa letu, familia
yetu, na zaidi sana moyo wangu. Ninakualika wewe uje moyoni mwangu uweze
kufunua kile kinacho kuhuzunisha wewe sana. Ninakualika uweze kukingoa ndani
yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment