MASOMO
YA MISA NOVEMBA 13, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 32 LA MWAKA
SOMO
1
Hek.
18:14-16, 19:6-9
Mambo
yote yalipokuwa kimya, na usiku ulikuwa katikati ya mwendo wake mwepesi, Neno
lako Mwenyezi alishuka mbinguni kutoka kiti chako cha kifalme, shujaa aliye
hodari, katika nchi iliyoposishwa hukumu, mwenye upanga mkali, ndio amri yako
isiyopindika, akasimama na kujaza mambo yote mauti, na pindi alipogusa mbingu
akaikanyaga nchi.
Kwa
maana ulimwengu mzima, kwa kadiri ya asili yake, ulifanyika tena mpya, kwa
kuzitii amri zako hizi na hizi, ili watoto wako walindwe wasipate dhara. Uwingu
ulionekana uliokitia uvuli kituo chao, nan chi kavu ikapanda kutoka pale
palipokuwapo maji kwanza, katika Bahari ya Shamu kukawa barabara isiyo na zuio,
na uwanda wenye majani katika mawimbi yaumkayo. Hapo watu wako wakapita pamoja
na majeshi yao yote, ambao kwa mkono wako walifunikwa, wakiisha kuona maajabu
makuu. Wakazunguka-zunguka huru kama farasi, wakaruka-ruka kama wana-kondoo,
wakikuhimidi Wewe, Bwana, uliyekuwa mkombozi wao.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
105:2-3, 36-37, 42, 43 (K) 5
(K)
Zikumbukeni ajabu Bwana alizozifanya.
Mwimbieni,
mwimbieni kwa zaburi,
Zitafakarini
ajabu zake zote.
Jisifuni
kwa jina lake takatifu,
Na
ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana. (K)
Akawapiga
wazaliwa wa kwanza katika nchi.
Malimbuko
ya nguvu zao.
Akawatoa
hali wana fedha na dhahabu,
Katika
kabila zao asiwepo mwenye kukwaa. (K)
Maana
alilikumbuka neno lake takatifu,
Na
Ibrahimu, mtumishi wake.
Akawatoa
watu wake kwa shangwe,
Na
wateule wake kwa nyimbo za furaha. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:105
Aleluya,
aleluya,
Neno
lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
18:1-8
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote,
wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji Fulani, hamchi
Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane,
aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda
alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,
lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha
kwa kunijia daima.
Bwana
akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu, je! Hatawapatia haki
wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia,
atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona Imani
duniani?
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment