“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Novemba 13, 2021.
Juma
la 32 la Mwaka
Hek
18: 14-16; 19: 6-9;
Zab
105: 2-3, 36-37, 42, 43;
Lk
18: 1-8.
KUVUMILIA
UKIWA KATIKA SALA!
Ndugu
zangu wapendwa, karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana katika asubuhi ya leo tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza. Hapa
tunakutana na mwandishi wa kitabu cha Hekima ya Sulemani akiongea na watu
wanaojiona kuwa ni wanyonge katika taifa jingine, yaaani Wayahudi wakiwa mjini Alexandria.
Huko wanakejeliwa na wanaphilosophia kama akina Epicureans(wanao amini maisha
ni hapa duniani tu, hivyo ponda raha iwezekanavyo, wala usijihusishe na maskini
kwani watakuletea shida zao na hapo utashindwa kuponda raha).
Lakini
mwandishi anawafundisha juu ya silaha wanayopaswa kutumia ili kukabiliana na
hawa watu. Anawaambia waendelee kungangania hekima ya Mungu. Hii ndiyo
iliyomwezesha Musa kufanya miujiza yote na kuwawezesha waisraeli kuvuka bahari
ya shamu na kuwaokoa katika mapito yote. Hekima hiyo hiyo ndiyo iliyowaangamiza
Wamisri kwa ile miujiza na walipokuwa katika bahari ya shamu. Sasa mwandishi
anawaambia waitafute silaha hii nao wataweza kuishi, hata kupambana na kejeli
za Epicureans.
Katika
injili tunakuta na mwendelezo wa kitu kama hiki. Yesu anamfundisha silaha
anayopaswa kuwa nayo yeyote aliye na Imani-na anayesumbuliwa na mapito ya
kimaisha kama hawa Wayahudi walipokuwa huko Alexandria. Anawaambia kwamba
wanapaswa kuwa na uvumilivu katika sala. Hii ndiyo hekima na silaha ya mnyonge,
hii ndiyo itakayomwezesha kuvuka katika mapito yote.
Tunaalikwa
kutumia silaha hizi kama Ayubu alivyotumia ile yake ya uvumilivu kupita mapito
yake, kama Daudi alivyotumia Imani yake kupita mapito yake kumshinda Sauli na
kama Abrahamu alivyotumia Imani yake kupita mapito yake hata kwenda nchi
asiyoijua aliyotumwa na Mungu.
Sasa
Yesu anatuambia katika injili kutafuta silaha zetu na kuzitumia katika kuvuka.
Yesu anatuambia kwamba nasi tukitumia silaha ya uvumilivu, tutashinda, tutavuka
na kuingia palipo pakavu kama wanawa Israeli walivyoweza kuvuka katika bahari
ya shamu.
Hivi
ndivyo Imani yetu inavyotudai ndugu zangu na ndizo silaha tunazopaswa kutumia.
Ukizikataa silaha hizi, nakwambia itakuwa ni majanga tu katika maisha. Kwani
maisha yana mapito mengi, kuna hali mbalimbali zinazojitokeza katika maisha.
Unaweza kujiona unacheka sasa, lakini kunatokea kitu na kufuta furaha zote.
Rafiki unayemtegemea au hata ndugu yako au hata mtoto anaweza kukutendea kitu
usichotegemea. Kama huna silaha kama hizi katika maisha yako au Imani yako kwa
kweli hutaweza kumudu uhalisia wa maisha.
Hata
sala yenyewe ilivyo: unajikuta wewe umepanga mipango yako namna hii, unataka
mambo yako yaende namna hii lakini Mungu anao mpango tofauti juu yako.
Anamipango yake tayari. Hivyo, pasipokuwapo uvumilivu katika Imani, utajikuta
kila siku unaishia katika kumlaumu Mungu. Hivyo ndugu zangu tujue silaha zetu
ni zipi na tuzikimbilie.
Tuzikimbilie
hasa tunapokutana na vitu vya ajabu katika Imani yetu. Unaposhangaa kuona
kwamba mwenzako kakutendea kitu cha ajabu katika maisha yako. Yaani, unakuta
mtu usiyemtegemea amekutendea kitu usichokitegemea kabisa. Sasa silaha hizi
zitakuwezesha kupita hapa.kuna wakati utadhaniwa vibaya na kudharaulika ndio
wakati wakutumia silaha kuhakikisha umebaki katika umoja na Mungu, kubaki
katika hiyo hekima ya Mungu, kwani matukano au vigelegele vya watu juu yako
havikufanyi wewe kuwa mbaya au kuwa Mtakatifu.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment