“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Novemba 25, 2021.
Juma
la 34 la Mwaka
Danieli
6:12-28
Zab.
100 (K) Ufu. 19:9
Lk.
21:20-28
Hizi
zitatufanya tuikose imani kwa hakika.
Karibuni
sana wapendwa wa Bwana kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana leo katika somo la kwanza tunapata habari juu ya imani ya Daniel. Aliweza
kuwa na imani kati kati ya wageni, wageni waliokuwa na roho mbaya juu yake,
waliotaka aikane imani yake. Hivyo walimzunguka kila upande kwa sababu ya imani
yake.
Leo
tunasikia wakimshtaki kwa mfalme ili uhai wake uondolewe. Lakini Mwenyezi Mungu
anakuwa upande wake. Daniel anamlimlia Mungu na kwa hakika anapata kuokolewa.
Matendo ya kufanyiwa fitina kama alivyofanyiwa Danieli wanafanyiwa wengi kwa
nyakati zetu.
Wapo
kati yetu wenye umbea, wenye kufuatilia mambo ya watu, tusiotaka watu waishi
bila uhuru, wafuatiliwe kila wanapokanyaga-kila wanachotenda kinaripotiwa-hakika
hizi sio tabia za kimungu. Wanadamu wanapaswa kuishi katika uhuru, hata kama ni
mke au mume anapaswa apewe uhuru na si kuishi kitumwa akifuatiliwa kama
mhalifu. Hivyo tuwe watu wa kuwapenda wenzetu waishi kiuhuru, tusiwabane sana
watu, tusiwe watu wa kutazama au kufuatilia kila kitu chao. Tabia za namna hii
zinatufanya tutende dhambi kila siku.
Binadamu
ni tofauti na simu yako au miguu yako ambayo kila wakati unapaswa kuitazama.
Wanadamu wameumbwa ili waishi kwa uhuru. Tukiwa na tabia za kufuatilia kila ya
mwenzetu hakika tutaishia kuwafitini na kuwaumiza wenzetu kila siku.
Katika
somo la injili, Yesu anaelezea juu ya ujio wa nyakati ngumu kwa mji wa
Yerusalem. Yerusalemu uliaminiwa kuwa mji wa amani lakini habari zinazoelezwa
juu yake leo kwa hakika ni tofauti, sio habari za amani. Yerusalemu ilishindwa
kupalilia amani yake kwa njia ya sala na kufanya toba na matendo mema. Mwishowe
amani yao inachezewa na wao kuishi katika huzuni. Nasi tujitahidi kutambua
kwamba tunaweza kuichezea amani yetu na kuishia kwenye magumu kama yaliyotokea
kwa Yerusalemu, mji uliotangazwa kuwa mji wa amani.
Hivyo
tusiwe watu wa kuendeleza siasa za chuki, za ukabila, unyanyasaji. Hizi
zitatufanya tuikose imani kwa hakika. Tujitahidi kukuza amani. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment