ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Oktoba 25, 2021.
Juma
la 30 la Mwaka
Rom
8: 12-17;
Zab
67: 2,4,6-7, 20-21 (K) 21;
Lk
13: 10-17.
YESU
ANAPONYA!
Yesu
alikuja huku ulimwenguni kwa ajili ya utume. Mojawapo ya utume huu ilikuwa ni
kuwaponya wagonjwa. Kila muujiza ulikuwa nitendo la upendo alilofanya Yesu kwa
mtu aliyeponywa. Leo utamuona mwanamke ambaye alikuwa akiteseka kwa miaka kumi
na nane na Yesu anamuonesha huruma kwa kumponya. Ingawaje ilikuwa nitendo la
upendo moja kwa moja kwake, kuna mengi ya kujifunza kwetu sisi. Huyu mwanamke
ambaye aliongozwa na Imani yake ilimfanya aende katika sinagogi na kukutana na
Yesu. Kwa kuona hili Yesu anachukua jukumu la kumponza.
Huyu
mwanamke katika hali ya kweli hakuwa anatafuta uponyaji, lakini Yesu alipomuona
moyo wake ulimsukuma na kwenda kumponya. Ni sawa na sisi pia tutambue Yesu
anajua tunahitaji nini, hata kabla hatujamuomba. Kazi yetu daima nikubaki
waaminifu daima kwake na tutambue kwamba katika uaminifu wetu atatupatia kile
tunacho hitaji hata kabla hatujamuomba.
Huyu
mwanamke alisimama imara alipo ponywa. Hii ni alama kuonyesha nini maana ya
neema kwetu. Wakati Mungu anaingia katika maisha yetu tunaweza tena kusimama
imara. Tunaweza kutembea tena tukiwa na nguvu mpya na utu mpya. Tunatambua sisi
ni wanani na tunaishi kwa uhuru katika neema yake.
Tafakari
leo, juu ya ujumbe wa Injili. Mungu anatambua kila kitu tunacho hitaji na
atajibu mahitaji hayo kadiri ya wakati wake. Na wakati atakapo tupatia neema
yake tutawea kusimama tena kama watoto wake. Tafakari, je kwenda kwetu kanisani
kunakuwa kama kwa yule mwanamke aliyeponywa? Au kwenda kwetu ni kwa ajili ya
matendo ya nje, kutazama makosa yaliotendwa na wenzetu wakati wa liturjia?
Sala:
Bwana, ninajikabidhi kwako na ninaamini katika huruma yako. Ninatumaini kwamba
utunisaidia mimi niweze kutembea katika njia yako kila siku ya maisha yangu kwa
ujasiri wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2021 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment