MASOMO
YA MISA OKTOBA 25, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 30 LA MWAKA
_____________
SOMO
1
Rum.
8:12-17
Kama
ni hivyo, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana
kama mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha
matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.
Kwa
kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa
hamkupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa
wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja
na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu
warithi; wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili
tupate kutukuzwa pamoja naye.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
68:1,3,5-6,19-20 (K) 20
(K)
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa.
Mungu
huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao
wamchukiao huukimbia uso wake.
Bali
wenye haki hufurahi,
Na
kuushangilia uso wa Mungu,
Naam,
hupiga kelele kwa furaha. (K)
Baba
wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu
katika ko lake takatifu.
Mungu
huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa
wafungwa wakae hali ya kufanikiwa. (K)
Na
ahimidiwe Bwana,
Siku
kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu
ndiye wokovu wetu.
Mungu
kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;
Na
njia za kutoka mautini. (K)
_____________
SHANGILIO
Ebr.
4:12
Aleluya,
aleluya!
Neno
la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya
moyo.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk.
13:10-17
Siku
ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama,
palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane,
naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita,
akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu
yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.
Basi
mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato,
akajibu akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni
mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akamjibu
akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, Je! Hamfungi ng’ombe wake au punda
wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye
wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii,
haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari
wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu
yaliyotendwa na yeye.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment