“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Novemba 1, 2021.
Juma
la 31 la Mwaka
SHEREHE
YA WATAKATIFU WOTE
Uf
7:2-4, 9-14;
Zab
23:1-6;
1
Yn 3:1-3;
Mt
5:1-12
WATAKATIFU:
WITO WA PAMOJA WA KUWA MTAKATIFU
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu.
Leo tunaadhimisha sherehe ya watakatifu wote na masomo yetu yanatualika vyema
kwenye kuitafakari siku hii ya leo. Zaburi yetu ya wimbo wa katikati inatuambia
juu ya kizazi cha wamtafutao Bwana na watakaoruhusiwa kupanda mlima wa Bwana.
Waliofanikiwa kuupanda huu mlima wa Bwana kuna Abrahamu, Musa na Elia.
Walipanda mlima wa Bwana na kukutana naye na kuongea naye na kupewa faraja
kubwa.
Habari
za watakatifu tunaowasikia katika somo la kwanza nao wamepanda mlima wa Bwana
na sasa wamekutana na Bwana na kufarijiwa naye na kuoshwa kila chozi machoni
mwao. Hawa walivaa mavazi meupe yaliyooshwa kwa damu ya mwanakondoo na
walipokuwa duniani walikubali kutiwa muhuri wa mwanakondoo na mkombozi na leo
wameshika matawi mikononi wakimshangilia mfalme wao Yesu Kristo.
Sisi
ndugu zangu tufuate njia yao. Kwanza tujikubali kutiwa chapa ya mwanakondoo
tukiwa hapa ulimwenguni kwanza kwa kukubali kubatizwa, kupokea sakrament
mbalimbali. Hapa tunajitia chapa na kujifunga kwamba sisi ni wakristo. Kila
mmoja leo aone umuhimu wa sakramenti katika kumtia chapa hii. Tuongeze bidii
kwa pale tulipoacha kuzipokea na tuache kasumba za kuwaacha watoto wetu bila
kubatizwa miaka na miaka.
Malaika
wa somo la kwanza anatudhihirishia kwamba siku hii ya watakatifu ni siku
inayoonyesha kupewa tuzo kwa wale waliopitia katika dhiki kuu na Yesu
analidhihirisha katika injili anapofundisha juu ya heri leo. Maisha ya heri
katika ulimwengu yanaonekana kuwa maisha ya kupitia katika dhiki kuu.
Waliomaskini wa roho-wasiongangania vitu au kuonyesha upole na kuishia
kudhulumiwa, wanaotafuta amani na kupigania haki. Watu wa namna hii wameishia
kudhulumiwa ndani ya ulimwengu huu.
Waliopigania
haki baadhi wameishia kuuawa na maadui. Hawa ndio waliopita katika dhiki kuu na
hakika leo wamepewa tuzo. Yesu hakika anakumbuka hata unywele wa kichwani
mwetu. Chochote tulichokitoa kwa ajili yake hakika atatutunza na kuturudishia.
Tusiogope kujitoa kwa ajili ya wengine. Tusiogope kupitia katika dhiki.
Waliopitia dhiki ndio wanatukuzwa leo. Sisi tusitake kupendwa na kuchekewa na
watu ili kubembeleza dhambi. Hawa waliopendwapendwa waliishia kukutana na
Lucifer kule motoni.
Heri
na baraka za Mungu kwa sikukuu ya somo wa kila mmoja wetu leo. Tutamani
utakatifu tukimbie dhambi.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment